Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, August 21, 2013

Jaji Mkuu Z’bar kusikiliza kesi mauaji Padri Mushi

jajimkuu_732e0.jpg
Kesi ya mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar, sasa itasikilizwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu.Hatua hiyo imekuja baada ya mshtakiwa anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya Padri Mushi, Omar Mussa Makame, kumkataa Jaji Mkusa Sepetu kwa madai ya kutomtendea haki.
P.T

Wakati kesi hiyo ikitarajiwa kuendelea, Arusha shauri la kutoa maneno ya uchochezi linalomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, jana limekwama kuendelea na kuahirishwa hadi Oktoba Mosi, kutokana na mshtakiwa kuwa mgonjwa.
Wakili Method Kimomogoro anayemtetea Lema, alimweleza Hakimu Mkazi, Devotha Msofe, kuwa mteja wake anaumwa malaria na homa ya tumbo na alikuwa amelazwa hospitali alikoruhusiwa Jumapili iliyopita.
Visiwani Zanzibar, Jaji Makungu akisikiliza kwa mara ya kwanza kesi hiyo ambayo ilianza Aprili 5, mwaka huu aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Omar Sururu Khalfan, alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika kutokana na kupelekwa vielezo kwa Mkemia Mkuu Dar es Salaam kwa uchunguzi na kwamba, havijarudishwa.

No comments:

Post a Comment