Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Breweries wakionesha muonekano mpya wa chupa ya Kibo Gold.
Meneja
Miradi endelevu na uwajibikaji kampuni ya bia ya Serengeti Nandi
Mwiyombela (Katikati), Meneja wa mauzo wa kanda ya kaskazini Patrick
Kisaka (kushoto) na Attu Mynah (kulia) kutoka idara ya mipango
wakionyesha mbele ya wasambazaji wa bia na waandishi wa habari aina mpya
ya chupa yenye shingo ndefu ambayo bia ya Kibo Gold itapatikana kuanzia
sasa, hafla hiyo ilifanyika katika kiwanda cha Serengeti Breweries
kilichopo mjini Moshi.
Meneja
wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella akizungumza
jambo mbele ya Wanahabari na wageni waalikwa kwenye hafla ya muonekano
mpya wa bia ya Kibo Gold
Meneja
wa kiwanda cha bia cha Serengeti cha njinpi Moshi Bw. Coleman Hanna
(katikati) akibadilishana mawazo na meneja mauzo wa kanda ya kaskazini
Bw. Patrick Kisaka (kulia) wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa bia
ya Kibo Gold uliofanyika kiwandani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Msambazaji
wa kwanza kabisa wa bia za Serengeti mkoa wa Kilimanjaro Mama Kisela,
akipokea bia ya Kibo Gold yenye muonekano mpya na ladha ileile kutoka
kwa Attu Mynah wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa wa bia hiyo
katika hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda hicho wmwishoni mwa wiki.
========= ====== =====
KAMPUNI YA BIA YA
SERENGETI YAFANYA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA KIBO.
SERENGETI YAFANYA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA KIBO.
*Sasa Kibo yang’ara katika chupa ya kisasa kabisa*
Kampuni
ya bia ya Serengeti leo imezindua muonekano mpya wa bia
inayosherehekewa sana mkoani hapa, Kibo Gold. Uzinduzi huu uliofanyika
katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Moshi, ulifikia kileleni
kwa shughuli murua iliyoandaliwa na kampuni hii na kushuhudiwa na
waandishi wa habari pamoja na wadau mbali mbali. Bia hii ya Kibo sasa
ina muonekano mpya wa chupa inayoashiria ubora wa kilichopo ndani. Bia
ni yenye ubora uleule wenye kiwango cha hali ya juu ila kwa chupa ya
rangi ile ile iliyongarishwa na shingo ndefu.
Akiongea
kwenye hafla hii Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi
Mwiyombella alisema bia hii ya Kibo Gold imekuwa ikitambulika kwa ubora
na ladha nzuri kwa wateja. “Kwa muonekano huu mpya wa chupa ya kisasa,
tunaamini wateja wengi watavutiwa na kuipenda zaidi
kwani ni muonekano unaokwenda na wakati. Ubora wa bia hii, unakuwa dhahiri kweli kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika kilele cha juu kabisa cha mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake hili la ‘KIBO’, aliongeza Bi Nandi.
kwani ni muonekano unaokwenda na wakati. Ubora wa bia hii, unakuwa dhahiri kweli kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika kilele cha juu kabisa cha mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake hili la ‘KIBO’, aliongeza Bi Nandi.
Kampuni
ya bia Serengeti chini ya kampuni mama ya Diageo, inazingatia kanuni
na sheria zilizowekwa na kampuni hii kwenye ubora katika uzalishaji wa
bidhaa zote. Muonekano wa bidhaa ni ule unaondena na soko za kimataifa
na wa kuvutia.
Kampuni ya bia ya Serengeti inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo.
Kampuni ya bia ya Serengeti inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo.
Kwa Mhariri:
Bia ya Kibo Gold ilirudishwa sokoni hapa Tanzania mwaka jana, 2012,
mwezi wa sita baada ya kuwa haipo kwenye soko kadri ya miaka kumi. Ni
mojawapo ya bia zinazoongoza nyanda za kaskazini sasa hivi. Bia hii
inazalishwa katika kiwanda cha bia cha Serengeti cha Moshi na
inasambazwa mkoani hapo na mikoa jirani, Arusha, Tanga, Manyara na Tanga
kwa wingi.
Tafadhali kunywa kistaarabu. Haiuzwi kwa walio chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment