Hapa unapo paona ndo hali ilivyokuwa majira ya saa 1 asubuhii ndani ya Nairobi.
|
Abiria wote wakiwa wanaamishwa kuelekea Hotelini...... |
|
Choka sana nishapamiss Bongo alafu haya ndo yanatokea nipo na mwanangu Moses Iyobo kuelekea Hotelini maana bado sijapata uhakika wa safari... |
|
Baada kama ya Lisaa hivi ya kukaa kwenye bus wameamua kutuleta hoteli maeneo ya huku huku Nairobi,Hoteli hii Inaitwa Panari(5star hotel) |
Niliwasili Alfajiri ya saa kumi na moja nikitokea nchini South Africa nilikuwa napita kubadilisha ndege kurejea nyumbani Bongo Lakini maswahibu haya yaliyotokea majira ya saa 1 asubuhi huku mimi na abiria wengine tukisubiri kwenye ndege ghafla tulikuja kujuzwa kuwa hali ya usalama pale Airport haikuwa shwari na tulivyotoka kwenye ndege ndio niliposhudia uwanja wa ndege wa Kenya ukiwaka moto.... Hadi sasa sasa chanzo cha moto ule uliosababisha kuwaka kwa Airport bado sijajua lakini hii imepelekea safari kukwama,sina uhakika kama tutaweza kuja Dar tena au Ndege kama zitaweza kuruka kwa leo maana hapa tulipo wanatupeleka hotelini, Imewalazimu Uongozi wa Immigration kuja na kutugonga mihuri kwenye basi la wasafiri na kuwekewa usalama wa mabegi yetu....
Zifuatazo ni Picha za Tukio zima Pale Airport ya Nairobi.....!! |
No comments:
Post a Comment