Walisema ndani ya gari hilo ambalo lilifungwa vioo, alikuwa na wenzake wawili ambapo ghafla walitokea vijana watatu waliokuwa na pikipiki aina yaToyo ambazo namba zake hazikufahamika wakiwa wameifunika na mifuko ya nailoni.“Walimgongea dirishani wakitaka afungue mlango, huyu mfanyabiashara hakufungua ndipo vijana hao walichomoa bastola na kuanza kugonga tena kwenye dirisha la gari.
“Walipoona hafungui, kijana mmoja alimimina risasi kwenye mlango wa mfanyabiashara huyo na zilimpata ubavuni, miguuni na tumboni...risasi nyingine ilimjeheruhi mwenzake Bw. Abel Musa, mwingine aliinama hivyo zilimkosa,” alisema.Waliongeza kuwa, baada ya vijana hao kufanya unyama huo, walifungua mlango na kuchukua mfuko wa rambo uliokuwa na zaidi ya sh. milioni 60 na kutoweka nazo kila mmoja akielekea upande wake.
Walisema baada ya tukio hilo, wananchi walikusanyika na kumchukua mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa vibaya na kumkimbiza hospitalini.“Inasemekana njama hizo zilipangwa na wafanyabiashara wenzake ambao waliwasiliana na majambazi na kuwaeleza mwenzao analipa madeni kwani alianza kuzunguka maeneo mbalimbali.Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kulisikia lakini hakuwa na maelezo hivyo aliahidi kulifuatilia zaidi
No comments:
Post a Comment