Na Walter Muguluchuma-mpanda
Mbunge
wa Jimbo la Mpanda mjini ambae pia ni Makamu wa mwenyekiti wa Taifa wa
chama cha CHADEMA Said Amour Arfi amefanyiwa upasuaji wa nyonga Nchini
India ambako alipelekwa kwa ajiri ya matibabu
Mdogo
wa Mbunge huyo Nassor Arfi alisema kaka yake alifanyiwa upasuaji hapo
juzi katika hospitali ya Apolo ya nchini humo baada ya kupewa rufaa
kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Alisema
Arfi aliondoka hapa Nchini Agosti 25 mwaka huu majira ya saa tisa
alasiri kwa ndege ya shirika la India akiwa amefuatana na mkewe ambapo
walifika siku hiyo hiyo na kupitiliza kwenye hospital hiyo.
Alifafanua kuwa mheshimiwa Arfi afya yake ilianza kuteteleka toka mwezi wa juni mwaka huu .
Mwihoni mwa wiki alipo pewa rufaa ya kwenda kutibiwa Nchini India
Mdogo
wake huyo alisema kuwa safari hiyo ya kwenda kutibiwa Nchini India
imegharamiwa na ofisi ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Alisema hari ya mbunge huyo baada ya kufanyiwa upasuaji huo wa nyonga inaendelea vizuri na kwa sasa ameanza kuongea
Mwaka 2011 mbunge huyo aliwahi kwenda nchini India kwa matibabu kama hayo mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2010
No comments:
Post a Comment