Taarifa iliyotolewa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom kupitia Ofisa Mkuu wa Mawasiliano, Georgia Mutagahywa ilisema moto huo uliozimwa, ulisababisha kusimama kwa huduma zote za kampuni hiyo.
“Tunawaomba radhi wateja wetu wote kutokana na usumbufu wa kukosa mawasiliano uliosababishwa na kuungua kwa vifaa muhimu vya kuendesha mitambo yetu,” alisema Mutagahywa.
Alisema, “Ninaomba niwahakikishie wateja wetu kwamba watarejeshewa huduma zote za vifurushi walizokuwa wamezinunua hapo jana pasipo kutakiwa kuzinunua upya pindi tutakapofanikiwa kurudisha huduma zote.” alisema Mutagahywa.
No comments:
Post a Comment