Na Gladness MallyaMSANII
wa filamu za Kibongo, Prisca Tadei hivi karibuni alinusurika kifo baada
ya kupata ajali mbaya ya pikipiki wakati alipokuwa akielekea ‘location’
kushuti.

Ajali
hiyo ilitokea wiki iliyopita maeneo ya Mbagala, jijini Dar ambapo
Prisca aliumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya pikipiki
aliyokuwa amepanda kugongwa na gari ambapo alikimbizwa Hospitali ya
Mnazi Mmoja na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.CHANZO GPL

Akichonga
na paparazi wetu, mkurugenzi wa kikundi anachofanyanacho kazi cha
Kalunde Entertainment, Mariamu Athuman ‘Kalunde’ alisema anamshukuru
Mungu kwa kuwa msanii wake huyo mpaka sasa anapumua na anaonesha
matumaini kwani ilikuwa ajali mbaya.
No comments:
Post a Comment