WANAMUZIKI
wawili wenye majina ya kutisha, Waziri Sonyo na Rais wa zamani wa bendi
ya Victoria Sound, wamepigana katika mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika
Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Waziri Sonyo kushoto.
Katika
kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo
kuzua hofu katika patashika ya aina yake inayoendelea kuonyesha mgogoro
mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya Victoria Sound.
Akizungumza
muda mchache baada ya kadhia hiyo, Muumini alisema alishangaa kujikuta
yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.
Muda
mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea
tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi
dhidi ya Sonyo.
“Leo ndio nimedhihirisha huyu (
hapa kuna tusi ila limefichwa kwa sababu za kiungwana) ni kweli yy
amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu
kunivamia sikumkawiza nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio
akaona kumbe huyu mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu ndio wakamshika
lakini wakati nakwepa kisu nilianguka kama sio George Gama
ameshanijeruhi au kuniua kabisa ngoja nimfunze adabu nampeleka
mahakamani ili iwe fundisho na kwa ili sina msalie mtume hivi jimwili
lote la Sonyo Bado anamshikia mwanaume mwenzie Kisu na amshukuru Janurry
aliyenipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikuwa kama kuku
mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kuipitia meseji ya Muumini.
Kupigana
kwa wanamuziki hao ni mwendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi
hiyo baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na
kumpa Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya
kiongozi wa shoo.CHANZO THECHOICETZ
No comments:
Post a Comment