THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Kikwete ateuliwa miongoni mwa watu mashuhuri
duniani
kujadili Utandawazi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa
kuwa miongoni mwa watu wachache mashuhuri duniani ambao watajadili Mawazo na Njia Mpya za Utandawazi wa Usawa
na Haki (New Ideas for a Fair
Globalisation) na jinsi Utandawazi unavyoweza kuendeshwa kwa usawa
zaidi na kunufaisha nchi zote duniani.
Watu
hao mashuhuri wameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki-Moon
na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Mheshimiwa Jose Barosso kujadili njia mpya ya
Utandawazi wa haki na usawa zaidi katika mkutano (retreat) wa watu wachache utakaofanyika katika Kijiji cha Alpbach,
Austria, kuanzia kesho.
Mkutano
huo wa siku mbili ambao utakuwa chini ya Wenyeviti Wenza Waheshimiwa Ban Ki-Moon
na Barosso utafanyika chini ya kivuli cha Taasisi ya European Forum Alpbach na Rais Kikwete ni kiongozi pekee wa Afrika
aliyealikwa kushiriki katika mkutano huo.
Mbali
na kushiriki katika majadiliano ya mada mbali mbali, Rais Kikwete amepangiwa
kuzungumza katika kikao cha ufunguzi pamoja na waheshimiwa Ban Ki Moon na
Barasso na pia kuzungumza katika kikao cha kufunga mkutano huo na wenyeviti
wenzao hao wawili pamoja na Rais wa Muungano wa Austria, Mheshimiwa Dkt. Heinz
Fischer.
Rais
Kikwete aliondoka nchini usiku wa jana, Jumatano, Agosti 28, 2013, kwenda
Alpbach tayari kwa mkutano huo ambao mada zake kuu zitakuwa ni Nishati Endelevu
na Mabadiliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula na Lishe na Elimu na Vijana.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
29 Agosti, 2013
No comments:
Post a Comment