Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 5, 2013

UNAMKUMBUKA MBABE WA MADEREVA DALADALA NA MAKONDA DAR?HUYU HAPA DAVID MWAIBULA



a6 cd3fd

Na ubabe wa maana ni ule ubabe wa kusimamia taratibu.
David Mwaibula alikuwa ni mmoja wa wababe wa Dar es salaam kwenye kusimamia taratibu. Juzi hapa nilikutana na kuongea naye kwenye moja ya vijiwe vya jijini Dar.

Hakika, jamaa alikuwa ni msimamizi mkuu na mahiri wa masuala ya Daladala jijini. Huyu alikuwa haswa ' Mzee wa Daladala'.

Mbali ya mabadiliko mengine, ndiye aliyeasisi utaratibu wa madereva na makondakta wa daladala kuvaa sare.

Na jamaa alikuwa mbabe haswa. Akimkuta kondakta amevaa kandambili alimshusha na kumwambia arudi nyumbani akafuate viatu vyake. Maana, kwa Mwaibula, mtu lazima uheshimu kazi yako. Huwezi kwenda kazini na kandambili.

Hakika, nchi kwa ujumla inahitaji kuwa na idadi fulani ya ' Wababe' wenye ujasiri wa kuanzisha mambo mapya na wenye kuhakikisha taratibu zinafuatwa. Na hapo nchi hiyo lazima itasonga mbele kimaendeleo.
CHANZO Maggid,

No comments:

Post a Comment