Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 22, 2013

UPDATE:PONDA HALI YAKE MBAYA...

.

SIKU chache baada ya kupelekwa Mahakama ya Kisutu, jijini Dar kisha Mahakama ya Mkoa Mrogoro kwa helikopta, hali ya kiongozi na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Shehe Ponda Issa Ponda imedaiwa kuwa mbaya.
Shehe Ponda Issa Ponda.
Agosti 19, 2013 saa 2:12, Shehe Ponda alifikishwa Mahakama ya Kisutu, Dar akitokea Gereza la Segerea ambapo alifutiwa mashitaka ya kuchochea vurugu nchini kati ya Juni 2
na Agosti 10, mwaka huu kwenye maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Morogoro.
Kama hiyo haitoshi, siku hiyohiyo alikimbizwa Morogoro kujibu mashitaka ya uchochezi aliyoyafanya katika mkutano wa hadhara hivi karibuni mjini humo, hali ambayo ilimfanya atoneshe kidonda chake cha risasi aliyodai kupigwa.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu, kutokana na jeraha hilo la risasi alilonalo kiongozi huyo, hekaheka alizozipata siku hiyo zilisababisha atoneshe kidonda na kumfanya ashindwe kusimama wala kulala hadi familia kufikia hatua ya kuomba arudishwe Hospitali ya Muhimbili katika kitengo cha mifupa (Moi) kwa matibabu zaidi.

“Kiukweli hali ni mbaya, wamempeleka harakaharaka tena ghafla, matokeo yake wamemtonesha kidonda. Tunaomba wamrudishe tena Moi (Muhimbili),” alisema mmoja wa ndugu wa familia aliyeomba hifadhi ya jina.


Akiwa Morogoro, alipandishwa kizimbani na kujibu shitaka la kwanza la uchochezi pamoja na mengine mawili anayodaiwa kuyafanya Zanzibar. Agosti 10, mwaka huu kwenye mhadhara uliofanyika Viwanja vya Shule ya Ndege, mjini Morogoro, Ponda alidaiwa kuchochea kwa kusema:
“Ndugu Waislamu msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa serikali.”
Shitaka hilo liliunganishwa na mengine mawili anayodaiwa kuyafanya Shehe Ponda maeneo ya Dar na Zanzibar

No comments:

Post a Comment