Baadhi ya wakazi wa Mivinjeni ufundi Kurasini
wamefunga barabara ya kilwa jijini dar es salaam kwa muda wa saa mbili
wakishinikiza kulipwa hundi zao na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo
ya makazi Profesa Anna Tibaijuka na kusababisha foleni kubwa ya magari.
Itv ilishuhudia sakata hilo ambapo wakazi hao
walikusanyika barabarani kwa kile kinachodaiwa kudai hundi zao ambazo
walikua walipwe hapo jana baada ya nyumba zao kuthathminiwa.
Wakazi hao wamesema kuwa serikali ilikubaliana na
mwekezaji kuwalipa pesa zao na kutaftiwa viwanja huko kibada lakini cha
kusikitisha zoezi la ulipaji hundi lilisitishwa hapo jana mpaka waziri
wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Prof Anna Tibaijuka atakapotoa
tamko lini walipwe.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akiongea
kwa njia ya simu na Itv amemuagiza Mkuu wa Wilaya watu hao kutawanywa
na yeyote atakayekaidi atachukuliwa hatua za kisheria kwani si taratibu
sahihi kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji barabara
hiyo ambao hawahusiki.CHANZO ITV
No comments:
Post a Comment