Beki wa Yanga, Kelvin Yondani (kushoto) akikwaana na wachezaji wa Sport Club Villa.
YANGA SC
leo imeibuka kidedea baada ya kuifunga Sport Club Villa ya Uganda mabao
4-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Mabao ya
Yanga yamefungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 7, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
dakika ya 27, Didier Kavumbagu dakika ya 30 na Haruna Niyonzima
kuhitimisha kipigo hicho kwa bao la 4 dakika ya 62. Bao pekee la Villa
limewekwa kimiani na Ndaula Moses dakika ya 18.
(Picha na Richard Bukos / GPL)
No comments:
Post a Comment