Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, September 23, 2013

AJALI MBAYA IRINGA LEO ABIRIA ZAIDI YA 50 WA SAI -BABA EXPRESS WANUSURIKA KIFO




Askari wa  usalama barabarani Iringa  wakilitazama  basi la kampuni ya  Sai - baba Express  lenye namba  za Usajili T 668 BCD ambalo  liligongana  uso kwa  uso na lori  la kampuni ya Ivori lenye namba T 280 ADK eneo la Kibwabwa  katika barabara  kuu ya  Mbeya - Iringa  mchana  wa leo na  watu  zaidi  ya  watatu  kujeruhiwa  vibaya na  wengine zaidi ya 50 ambao ni abiria  wa  basi hilo kunusurika kifo
Lori la kampuni ya Ivory lenye namba  za usajili T 280 ADK lililogongana na basi hilo
Mmiliki wa  Lori la Ivory akiwa kama amechanganyikiwa  kwa  kupiga picha kila kona la basi hilo huku abiria  wakishangaa
Abiria  wa  basi la Sai- Baba Express wakilitazama basi  walilokuwa  wakisafiria  kutoka Tunduma Mbeya Kwenda Dar  ambalo limepata ajali  mbaya eneo la Kibwabwa  barabara  kuu ya Mbeya - Iringa  mchana wa  leo

WAKATI  Taifa  likiwa katika maadhimisho ya  wiki  ya nenda  kwa  usalama barabarani ajali  mbaya  imetokea  katika  eneo la Kibwabwa barabara  kuu ya  Iringa - Mbeya  baada ya  basi la  Sai- Baba  Express  kugongana  uso kwa uso na lori  la kampuni ya Ivori mchana  wa leo.

 Basi  hilo la kampuni  ya  Sai - baba Express  lenye namba  za Usajili T 668 BCD ambalo  liligongana  uso kwa  uso na lori  la kampuni ya Ivori lenye namba T 280 ADK ndilo ambalo linatajwa  kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo.

Mashuhuda  wa ajali  hiyo  wameueleza mtandao  huu kuwa ajali  hiyo  imetokea majira ya saa 8 mchana  wakati  basi hilo  likitokea  mkoani Mbeya na  Lori hilo likitokea mjini Iringa  na hivyo kugongana  uso kwa uso  .

Mmoja kati ya abiria  wa basi  hilo Yusuph Juma alisema kuwa  dereva wa  basi hilo alikuwa katika mwendo kasi mbali ya  eneo hilo la mji  kuwepo alama  zinazokataza  spindi zaidi ya 50 ila bado basi hilo  lilikuwa katika mwendo zaidi .

Alisema  kuwa  mbali ya magari hayo kugongana  uso kwa  uso  ila bado  basi hilo  liliweza  kushindwa  kusimama na kulazimika  kusimama  zaidi ya  mita  200 kutoka eneo la ajali .

Hata hivyo alisema ni jambo la kushuruku Mungu  katika ajali hiyo mbali ya  dereva wa  lori kujeruhiwa vibaya wengine  waliojeruhiwa ni pamoja  na  utingo  wa  basi na abiria  mmoja  huku abiria  wengine zaidi ya 50  wakinusurika katika ajali  hiyo.

Viongozi  mbali mbali  wa  jeshi la polisi ,Sumatra  na mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani  mkoa  wa Iringa Bw  Salim Asas  ni miongoni mwa mashuhuda  waliofika  kushuhudia tukio  hilo ambalo limetokea  huku taifa  likiwa katika  wiki ya nenda kwa  usalama taifa yatakayodfanyika kitaifa jijini Mwanza kuanza  wiki ijayo  chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania . 


Source: www.matukiodaima.com

No comments:

Post a Comment