Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 18, 2013

AZAM WAJIANDAA KUWALAMBISHA KONI ASHANTI UNITED leo

azam 22b7e
MAKAMU bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Azam fc inajiandaa kuvuna pointi tatu muhimu katika mchezo wa kesho dhidi ya Ashanti United , 'Watoto wa jiji' , uwanja wa Azam Complex baada ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera jumamosi ya wiki iliyopita. (HM)

Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema kocha mkuu wa klabu hiyo Sterwart John Hall ameshabaini makosa yaliyomnyima ushindi katika mchezo uliopita, hivyo anaendelea kuyafanyia kazi kabla ya kibarua cha kesho.
"Hatujaanza vizuri ligi msimu huu, tumetoa sare mbili na kushinda mechi moja, si matokeo mazuri kwetu, lakini mpira wa miguu ni mchezo wa makosa, kikubwa tuko tayari kwa mechi ijayo na watoto wa jiji, Ashanti United, Kocha wetu anafanyia kazi makosa ya vijana wake". Alisema Jafar.
Jafar alisema baada ya kubanwa na Kagera Sugar, wamegundua kuwa ligi ya mwaka huu ina ushindani mkubwa na hata ukiangalia wanaoongoza kileleni nje ya timu nne za juu msimu uliopita.
"Azam fc ni klabu iliyofanya maandalizi mazuri, tunahitaji kushinda mechi ijayo ili kuendelea kujipanga kuingia rasmi katika ushindani wa kuwania taji msimu huu". Alisema Jafar.
Afisa habari huyo aliongeza kuwa nia ya Azam siku zote ni kuleta mapinduzi ya soka, hivyo wanaendeleza mipango hiyo kwa kuhakikisha kikosi chao kinakuwa bora muda wote kutokana na kusheheni makocha wazuri na wachezaji wenye uwezo na morali kubwa.
Kwa sasa Azam fc wapo nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi tano kibindoni, ambapo mchezo wa kwanza walitoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar uwanja wa Munungu, mchezo wa pili walishinda mabao 2-0 dhidi ya Rhino Rangers mjini Tabora na mechi ya tatu wakatoka sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar juzi mjini Bukoba mkoani Kagera.
Msimu uliopita Azam fc walitwaa nafasi ya pili na kuliwakilisha taifa katika michuano ya kombe la shirikisho na kufika hadi Raundi ya tatu na hatimaye kutolewa kwa mbinde na AS FAR Rabat ya Morocco. Chanzo: Baraka Mpenja

No comments:

Post a Comment