Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na
kusalimiana na wananchi Wilayani Maswa mara baada ya kuwasili akitokae
Shiyanga, ambapo anaendelea na ziara yake ya kuimarisho chama kukagua
miradi ya maendeleo na katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama
hicho ambapo leo baada ya shughuli mbalimbali atawahutubia wananchi
mjini Maswa Mkoa mpya wa Simiyu jioni hii.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi , Siasa na Uenezi akishiriki kuchanaganya
mchanga wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua
ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ghami Kata ya Nyalikungu Wilayani
Maswa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua
matofali kwa ajili ya ujenzi ujenzi wa zahanati ya Ghami Katika kata ya
Nyalikungu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua tofali alilolifyatua wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa zahanati hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua akizungumza na
wananchi wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa Zahanati katika kijiji
cha Ghami Kata ya Nyalikungu Wilayani Maswa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na wanaCCM
wa shina la Komalija mjini Maswa mara baada ya kuongea nao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa shina la muungano Wilayani Maswa.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MASWA SIMIYU)

No comments:
Post a Comment