Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 10, 2013

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMA​N KINANA AWASILI NZEGA



120 31b34
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye ukiwasili katika mji wa Nzega  Tayari kwa kuanza Ziara ya Siku 18 katikia mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara kesho ambapo ziara hiyo itaanza katika mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu huyo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na wananchi waliojitokeza katika mapokezi hayo, Kinana leo amezungumza na wananchi wa Nzega na kukutana na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ambapo pia amepokea Pikipiki tisa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Dk. Khamis Kigwangala ambazo ambazo amezikabidhi kwa viongozi wa kata 9 kati ya 21 zilizopo katika Wilaya hiyo, ambapo pia amekabidhi mashine ya kutotolea vifaranga vya kuku kwa kikundi cha wazee wa Nzega , Pikipiki hizo zimekabidhiwa katika kata za Budushi, Ndala, Puge, Nkininziwa,Mbogwe, Lusu, ,Ijaniga, Utwigu na Isanzu baadae pikipiki 7 zitafutaiwa na kisha kata tano za mwisho. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-NZEGA

No comments:

Post a Comment