Baadhi ya waandishi wa
habari waliohudhuria mkutano huo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
Jijini Dar es Salaam leo.
(Picha zote na Hassan Silayo)
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTOAJI LESENI ZA BIASHARA CHINI YA SHERIA YA
LESENI ZA BIASHARA NA. 25 YA 1972 KWA MFUMO WA KUHUISHA NA KULIPIA ADA
1. UTANGULIZI
Serikali ilirudisha rasmi utozaji
wa ada za Leseni za biashara kupitia Sheria ya Fedha Na.5 ya mwaka 2011.
Maandalizi yamekuwa yakifanyika kutoka wakati huo na ada zimeanza kutozwa rasmi
01/07/2013 kwa mfumo wa kuhuishwa (Renewal).
Kutokana na marekebisho hayo,
utaratibu wa kutoa Leseni za Biashara BILA
MALIPO uliondolewa na kusitishwa na Serikali tarehe 30 Juni, 2013. Leseni
za Biashara zilizotolewa kuanzia tarehe 1 Julai, 2004 hadi 30 Juni, 2013 ambazo hazikuwa na UKOMO zinatakiwa kupelekwa kwenye
Mamlaka zilizotoa Leseni hizo, ili zihuishwe na kulipiwa ada kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa
Serikali.
Kila mfanyabishara mwenye Leseni ya Biashara anapaswa kujaza Fomu ya Maombi
ya Leseni ya Biashara na kuambatisha
Leseni ya Biashara aliyonayo na kuiwasilisha katika Mamlaka husika, kwa ajili
ya kuhuisha na kulipia ada. Maombi yapelekwe
katika Mamlaka iliyotoa Leseni husika. Kwa Leseni za Biashara za kundi “A” kama
ilivyoainishwa kwenye Fomu ya Maombi ya Leseni
ya Biashara TFN Na. 211ya 2004 hutolewa na Wizara ya Viwanda na
Biashara. Maombi hayo yawasilishwe katika
Ofisi za Wizara ya Viwanda na Biashara
zilizopo Barabara ya Sokoine Jengo la
NSSF-“Water front”, Ghorofa ya Nne chumba Na. 416. Kwa wale Wafanyabiashara wa
Kundi “B” kama ilivyoainishwa kwenye Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara TFN Na. 211ya 2004 wafike Ofisi
za Halmashauri za Majiji, Manispaa na
Wilaya zilizo katika maeneo yao, watapata huduma kutoka kwa Maafisa Biashara wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa.
2. UTARATIBU WA KUFUATA ILI KUFANIKISHA ZOEZI
NA KUPATA HUDUMA KWA HARAKA
- Kwa wafanyabiashara wa Kundi “A” wajaze Fomu ya Maombi ya Leseni za Biashara (fomu inapatikana katika tovuti ya Wizara sehemu ya Marketing Sector (www.mit.go.tz) au fika Wizarani NSSF-Waterfront ghorofa ya 4 chumba Na. 416, Kwa Wafanyabiashara wa Kundi “B” wawasilishe maombi Ofisi za Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya zilizo katika maeneo yao;
- Waambatishe Leseni za Biashara za kudumu walizonazo na kuwasilisha kwenye Mamlaka husika kama ilivyoainishwa hapo juu;
- Kwa wafanyabiashara wa Kundi “A” wafanye malipo kupitia Benki ya CRDB mahali popote kwa kutumia Account Number 0150413356300; jina Revenue Collection Trading License-MIT. Wafanyabiashara wa Kundi “B” wataelekezwa Benki ya kulipia na Halmashauri zao;
- Kwa wafanyabiashara wa Kundi “A” wawasilishe “pay slip” ya Benki ghorofa ya Mezanine (NSSF-WaterFront) kwaajili ya risiti ya Serikali, Wafanyabiashara wa Kundi “B” wataelekezwa Ofisi ya kuwasilisha ili wapewe reisiti ya Serikali-Mweka Hazina wa Halmashauri;
- Kwa wafanyabiashara wa Kundi “A” wawasilishe Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara, Leseni ya Biashara na risiti ya malipo ghorofa ya 4 kwa ajili ya kuandikiwa Leseni ya Biashara, Wafanyabiashara wa Kundi “B” wataelekezwa ofisi ya kupeleka na kuandikiwa Leseni ya Biashara ofisi za Biashara za Halmashauri.
Waombaji wapya wa Leseni za Biashara
mnapaswa kujaza fomu ya maombi ya Leseni za Biashara na kuambatisha
nyaraka kama inavyojieleza katika fomu ya maombi na kufuata hatua ya 1 hadi 5
kama ilivyoelezwa hapo juu.
Mnashauriwa kuhuisha na kulipia ada Leseni za Biashara mapema kabla ya
tarehe 31 Desemba, 2013 ambapo adhabu na
faini kwa wafanyabiashra watakaochelewa kuhuisha (Renew) itaanza kutolewa tarehe 1 Januari, 2014.
- TAHADHARI
Wafanyabiashara mnatadharishwa kuwa hapa mjini
kuna mawakala wasio waaminifu maarufu kwa jina la VISHOKA. Mnashauriwa kuwaepuka
na muweke utaratibu wa kufuatilia Leseni za Biashara zenu wenyewe.
Kwa wale ambao, wameshaletewa
Leseni za Biashara na mawakala waliowatuma mnashauriwa kwenda kwenye Mamlaka
iliyotoa Leseni husika kwa ajili ya kufanya uhakiki kwa kuwa imebainika kuwa
kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya biashara kwa kutumia Leseni batili
(Feki)
TAFADHALI FIKA NA KUFANYA UHAKIKI KWA FAIDA YA BIASHARA YAKO.
MAELEZO ZAIDI YANAWEZA KUPATIKANA PIA KWA KUTUMIA ANUANI IFUATAYO:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Viwanda na Biashara,
S. L. P. 9503,
Simu
Na-+255-22-2127897/8,
Fax:
+255-22-2125832
Website
– www.psmit.go.tz
DAR ES SALAAM.
WIZARA YAVIWANDA NA BIASHARA
No comments:
Post a Comment