MECHI YA SIMBA, MTIBWA YAINGIZA MIL 102/-
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa
jana (Septemba 14 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 95,080,000.
Watazamaji
16,507 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 15 ya VPL msimu wa
2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao
2-0.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,018,077.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,503,728.81.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,704,107.18,
tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 7,022,464.31, Kamati ya Ligi
sh. 7,022,464.31, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,511,232.15 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,730,958.34.
MJINI MAGHARIBI MABINGWA COPA COCA-COLA
Mjini
Magharibi imetwaa ubingwa wa michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 15 upande wa wavulana baada ya jana (Septemba
14 mwaka huu) kuifunga Ilala bao 1-0.
Mechi
hiyo ya fainali ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es
Salaam. Ilala iliwavua ubingwa Morogoro baada ya kuwafunga kwenye mechi
ya nusu fainali kwa kuivua ubingwa Morogoro katika mechi iliyoamriwa kwa
mikwaju ya penalti.
Kwa
upande wa wasichana, Mwanza ndiyo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwa
njia ya penalti dhidi ya Ilala. Hadi muda wa kawaida wa mchezo huo
uliochezwa jana (Septemba 14 mwaka huu) jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, jijini Dar es Salaam timu hizo zilikuwa suluhu.
No comments:
Post a Comment