Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 25, 2013

WAWILI WAKAMATWA WAKIWA NA MAITI YENYE MADAWA YA KULEVYA





Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la RAJAB KANDUNDA amekutwa akiwa amefariki katika nyumba moja kwenye chumba kinachomilikiwa na NASRI OMARI huku akiwa na dawa za kulevya tumboni katika eneo la Tabata jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam DCP SULEIMAN KOVA amesema jeshi hilo limepata taarifa za kuwepo kwa maiti hiyo kutoka kwa wasamaria wema na kufuatilia ambapo walifanikiwa kumtia mbaroni mmiliki wa chumba alipokutwa maiti huyo na mke wa marehemu.

Baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao maiti ya RAJAB KANDUNDA ambayo pia ilikutwa na pipi 33 za Heroin ilichukuliwa na polisi kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi.

Wakati huohuo,Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamishna wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleimani Kova amesema ugunduzi huo ulibainika baada ya uchunguzi uliofanywa na madaktari wa hospitali ya taifa Muhimbili wakishuhudiwa na polisi pamoja na baadhi na ndugu wa marehemu ambapo ameelezea marehemu alikutwa na hati za dharura za kusafiria nchi za nje na kuwa uchunguzi zaidi unafanyika kubaini mtandao mzima wa usafirishaji wa dawa hizo uliomuhusisha marehemu.

Katika tukio lingine kamanda Kova amesema jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja aliyejifanya kuwa mtumishi wa wizara ya afya na ustawi wa jamii aliyekamatwa katika hospitali ya taifa Muhimbili akiwa amevalia mavazi ya kidaktari pamoja na nyara mbalimbali zenye nembo ya hospitali hiyo kwa lengo la kuwaibia watu.

Kutokana na tukio la ugaidi nchini Kenya kamanda Kova amesema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulizi maeneo yote yenye mkusanyiko wa watu wengi na kutoa wito kwa jamii kuendelea kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi watakapo baini mtu au kikundi cha watu wanaowatilia shaka.

No comments:

Post a Comment