Diwani wa kata ya Majimoto Tarafa ya Mpimbe wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Nyasongwe Serengeti akiwa amelazwa katika wodi namba moja katika hospitali ya wilaya ya Mpanda akiwa katika hali mbaya baada ya kupokea kipigo toka kwa askari wanaofanya opareshen kimbunga inayoongozwa na jeshi la wananchi kufuatia vurugu zilizotokea hapo juzi katika kijiji cha Luchima baina ya askari hao na wanakijiji hicho ambapo katika tukio hilo mwanakiji mmoja aliuwawa kwa kupigwa risasi na mwingine kupigwa risasi mguuni ambapo mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia ASP Mafie alijeruhiwa kichwani kwa fimbo na kupoteza Fahamu na wanakijiji hao ambao alilishambulia gari la polisi lenye namba za usajili PT 0985.
Picha na Walter Mguluchuma-Katavi yetu Blog
********
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Diwani
wa Kata ya Majimoto Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi Nyasongwe (45) amejeruhiwa vibaya na kulazwa
hospitalini baada ya kupigwa na askari wanaofanya oparesheni kimbunga
katika Mkoa wa Katavi wakati akiwa msibani kwa mwanakijiji aliye uwawa
kwa kupigwa risasi na Askari wanaofanya oparesheni kimbunga baada ya
kutokea vurugu baina yao na wanakijiji cha Luchima kata ya Majimoto
Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi
Akiongea kwa taabu na waandishi wa
habari Diwani huyo wa Kata ya Majimoto ambae amelazwa katika wodi
namba moja huku akiwa chini ya ulinzi wa Polisi katika wodi namba
moja katika hospitali ya wilaya ya Mpanda ambako amelazwa toka juzi
mchana
Alisema tukio hilo na kupigwa na kujeruhiwa
lilitokea hapo oktoba 13 mwaka huu majira ya saa sita mchana wakati
akiwa msibani kijijini hapo alipokuwa amekwenda kwenye msiba wa
mwanakijiji ambae alikuwa ameuwa muda mfupi kwa kupigwa risasi na
askari wanaofanya opuresheni Kimbunga
Alieleza kuwa siku hiyo ya tukio yeye
wakiwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mamba Lyoba Juma Shomari walipata
taarifa kuwa kumetokea vurugu baina ya wanakijiji cha Luchima na Askari
wanaofanya opuresheni Kimbunga na kusababisha kifo cha mwanakijiji
mmoja na kushambuliwa na kujeruhiwa kwa mkuu wa kituo cha kutuliza
ghasia wa Mkoa wa Katavi ASP Mafie
Diwani huyo ambae ameumia vibaya sehemu ya
matako alisema ndipo walipokubaliana na afisa tarafa huyo na
kuelekea kwenye eneo la tukio ambapo walikuta wanakijiji wakiwa
wameweka tayari msiba wa mwanakijii mwenzao ambae alikuwa ameuwawa kwa
kupigwa risasi
Alifafanua kuwa kifo cha mwanajijiji huyo
kilitokana na vurugu zilizotokana na wanakijiji hicho kutoridhishwa
kuona mwenzao mmoja nyumba yake ikipekuliwa na kikosi cha opareshen
kimbunga ndipo walipoamua kumshambulia kwa fimbo ASP Mafie na
kujeruhi kichawni na kumfanya kupoteza fahamu
Pia wanakijiji hao walilishambulia kwa mawe
gari la polisi lenye namba PT 0985 na kulivunja kioo ndipo askari hao
wa opuresheni kimbunga walipo amua kufyatua risasi ambayo ilimuuwa
mwanakijiji huyo na kumjeruhi mguuni mwakakijiji mwingine ambae
amepelekwa Katika hospitali ya Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ajiri ya
matibabu
Serengeti alieleza kuwa wakati wakiwa bado
wako hapo msibani ghafla lilitokea kundi la askari wa opuresheni
kimbunga na kuanza kuwashambulia waombolezaji wote waliokuwepo hapo
bila kujali jinsia ingwa yeye na afisa Tarafa hiyo waliweza
kujitambulisha lakini waliendelea kupokea kipigo bila huruma kutoka kwa
askari hao
Alieleza kuwa kisha walipakiwa kwenye roli
la jeshi wakiwa na kundi la watu waliokuwa wanaomboleza msibabani
hapo kwa kudaiwa kumshambulia mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia wa
Mkoa wa Katavi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari alipotakiwa kutowa ufafanuzi kuhusiana na tukio
hili alisema kuwa opuresheni hiyo Kimbunga mhusika ambae anatakiwa
kutowa taarifa za tukio hili ni mkuu wa Hifadhi ya wanyama pori ya
Katavi
Kwa upande wake mkuu wa Hifadhi ya Katavi
Ignasi Gara alishindwa kutowa kabisa ushirikiano kwa waandishi wa
habari na kuatupia jeshi la wananchi kuwa wao ndio wasemaji wakuu
Na Katavi yetu Blog
No comments:
Post a Comment