Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (Kamati ya Ligi) wameeleza kuunga mkono utaratibu huu makini.
"Baada ya kupata haki za matangazo ya
luninga ya Ligi Kuu ya Vodacom, moja ya shabaha zetu kuu imekuwa ni
kuhakikisha kuwa tunafanikiwa kurusha matangazo yanayokidhi viwango vya
kimataifa kwa ubora. Ili kufanikisha shabaha hiyo tumewekeza vilivyo
katika teknolojia ya kisasa ya vifaa vya matangazo ya nje (Outside
Broadcasting) na katika mafunzo kwa watumiaji wa vifaa hivyo. Ninayo
furaha kusema kuwa matayarisho yamekwenda vema kiasi kwamba tumejikuta
tuko tayari kurusha matangazo ya kiwango cha juu kabla hata ya
kuzinduliwa kwa huduma kamili za AzamTV", alisema Rhys Torrington, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited.
"Kwa kuwa mashabiki wengi kote nchini wanangojea kwa hamu kubwa kuziona timu wazipendazo, imeonekana ni vema kuanza kuonesha michezo hii ya Ligi sasa. Kwa kuzingatia hali hiyo, nilifanya mazungumzo na rafiki zetu pale TBC na kuwaomba iwapo wana uwezo na kuridhia kurusha matangazo yetu ya moja kwa moja bila ya malipo yoyote kuanzia mwisho wa juma hili hadi kukamilika kwa nusu msimu. Tulifanikiwa kufikia makubaliano kwa haraka na sasa tunafanyia kazi masuala ya kiufundi yatakayowezesha kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi utakaofanyika Uwanja wa Taifa", Aliongeza Bw. Torrington.
Mara tu huduma kamili za AzamTV zitakapozinduliwa majuma machache yajayo, matangazo ya michezo ya Ligi Kuu kwa wigo mpana yatakuwepo pia kwenye chaneli yake hadi mapumziko ya nusu msimu. Baada ya hapo matangazo ya Ligi Kuu ya Vodacom yatapatikana kwa wale tu watakaokuwa na visimbuzi (decorders) vya AzamTV.
Chanzo:Shaffihdauda

No comments:
Post a Comment