Mtoto Ismail Godfrey akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.
MWANAFUNZI
wa darasa la sita, Ismail Godfrey (13) anayesoma katika Shule ya Msingi
Maendeleo Sinuka iliyopo mkoani Kigoma amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudai kutandikwa viboko na Mwalimu Muige Joseph na kupooza miguu.
Mtoto
huyo ambaye kwa sasa anapata matibabu katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jijini Dar baada ya kukosa matibabu ya kina mkoani Kigoma
alipokutana na mwandishi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Awali sikuwa na matatizo yoyote ya kiafya hususan katika viungo vya
mwili, isipokuwa haya yalinipata baada ya kuchapwa fimbo na mwalimu
wangu ndipo nikapooza ghafla.
Miguu ya mtoto Ismail iliyopooza.
“Tukio
hili lilitokea mwezi wa tano nilipokuwa shuleni, nilipofika nilifungua
bomba nikawa nakunywa maji kwa kuwa nilikuwa na kiu, ghafla mwalimu huyo
alikuja na kuniambia kwa nini nachezea boma, ndipo akaanza kunitandika
viboko.“Hapo hapo nikahisi viungo vyote vya mwili vimepoa na miguu ikapata ganzi, nikaanguka chini baada ya kukosa nguvu,” alisema Ismail.
Kutokana na tukio hilo baba wa mtoto huyo, Godfrey Lucas aliitwa na
baada ya kuona Ismail yupo katika hali hiyo ya kupooza miguu aliamua
kumpeleka katika Hospitali ya Mkoa, Maweni, kupatiwa matibabu, huku
akifanya juhudi za kumtafuta mtuhumiwa ambaye alikuwa amekimbia makazi
yake.
Ismail Godfrey.
Hata
hivyo , kutokana na juhudi za kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi
walifanikiwa kumkamata mwalimu huyo katikati ya mji wa Kigoma na
kumfikisha polisi ambapo alifunguliwa kesi kwa jalada namba
KIGO/RB/2269/013 17/3/2013 SHAMBULIO LA MWILI.
“Mtoto alianza kutokwa na vidonda miguuni ndipo nikaamua tuje hapa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na tukapokelewa na mtoto amelazwa
wodi ya wagonjwa ya Kibasila,” alisema.
Hata hivyo, amesikitika kuachiwa mtuhumiwa kwa dhamana wakati mwanaye bado kalazwa na anakosa masomo kwa sababu yake
No comments:
Post a Comment