Kikao cha baraza la madiwani la hamshauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza leo kimetawaliwa na vurugu na mabishano hali iliyopelekea kuvunjika kwa kikao hicho.
Vurugu na kurushiana maneno makali, zilianza baada ya meya wa halmashauri ya wilaya hiyo, Henry Matata kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo alipotoa amri ya kuwafukuza kwenye kikao madiwani wawili kutoka chama cha Demokrasi na maendeleo (chadema).
Meya huyo ambaye mefungua kesi mahakamani ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chadema, aliwataka madiwani hao kutoka nje kwa kile alichoeleza kuwa alikwisha wavua wadhifa wa udiwani kwa kitendo chao cha kugomea kuhudhuria vikao vya baraza bila kuiomba ruhusa kwa meya huyo
Vurugu hizo zilipelekea kushindwa kufanyika kwa kikao hicho ambapo madiwani hao wameeleza masikitiko yao kwa serikali kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Meya huyo.CHANZO JAMII FORUM
SUGECO KUBADILI MAISHA YA WAKULIMA KIJIJI CHA LUBONGO MVOMERO
-
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka vijana katika
kijiji cha Lubungo kuchangamkia fursa za uwekezaji ...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment