Nairobi.
Picha zilizonaswa kupitia kamera za CCTV zilizofungwa kwenye jengo la
kibiashara la Westgate Mall mjini Nairobi zinaonyesha kwamba magaidi
waliov
amia jengo hilo walikuwa wanne, hivyo kuanza kuibua mtizamo mpya kuhusu magaidi waliovamia jengo hilo.
Kwa
mujibu wa shirika la habari la AP, taarifa hizo ambazo bado si rasmi
kutoka kwa mmoja wa maofisa wa juu wa Serikali ya Kenya juzi, zilieleza
kwamba watu wanne wakiwa na silaha za kisasa ndio walioonekana kupitia
kamera hizo za siri, hivyo kuanza kuwepo kwa uwezekano wa kupungua kwa
idadi ya awali ya watuhumiwa hao wa ugaidi waliovamia jengo hilo.
Awali,
Serikali ya Kenya ilieleza kwamba wavamizi hao ambao walijitambulisha
kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la Al Shabaab la Somalia waliotekeleza
uvamizi huo Septemba 21, walikuwa kati ya 10 hadi 15 na kusababisha vifo
vya watu 67, idadi ambayo imeanza kutiliwa walakini.
Kati
ya waliouawa, kwa mujibu wa taarifa za Serikali, walikuwemo wanausalama
sita, watatu wakiwa maofisa usalama wa jeshi na watatu wakiwa maofisa
usalama wa polisi ambao waliuawa kwati wa kujibizana risasi walipokuwa
wakijaribu kuwadhibiti wavamizi hao.
Taarifa
hizi zimeanza kuvuja wakati wataalamu wa masalia ya miili ya binadamu
wakiendelea kufanya uchunguzi kwenye mabaki ya miili ya watu waliokuwa
wamenasa kwenye vifusi vya jengo hilo.
Wakati
uchunguzi huo ukiendelea, tayari vijana kadhaa wameshakamatwa kwenye
eneo la watu wa makazi duni la majengo mjini Nairobi, kwa ajili ya
kufanyiwa mahojiano kama sehemu ya polisi kujaribu kuwanasa wavamizi hao
ambao kwa mujibu wa taarifa za awali, walifanikiwa kutoroka kupitia
mtaro wa maji machafu unaotoka kwenye jengo hilo.
HII NI VIDEO IKIONYESHA PICHA ZA KAMERA YA CCTV NDANI YA JENGO
LA WESTGATE MALL.
.
No comments:
Post a Comment