COASTAL Union ambayo ni miongoni mwa timu zilizosajili kwa
gharama msimu huu, imemtimua Kocha Mkuu Mzanzibari, Hemed Morocco, kwa
madai ya kutoridhishwa na kiwango cha uchezaji wa timu hiyo.
Timu hiyo ina pointi 11 sawa na Kagera Sugar
wakiwa na tofauti ya mabao na inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa
Ligi Kuu Tanzania Bara. Imeshacheza mechi nane, ikashinda mbili, kutoka
suluhu tano na imepoteza mchezo mmoja dhidi ya timu dhaifu, Ashanti.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Edo Kumwembe,
aliliambia
Mwanaspoti kuwa uongozi wa klabu yake ambao ulikutana juzi Jumanne, umefikia azimio la kutomwongezea Morocco mkataba baada ya ule wa awali kumalizika tangu Septemba 31.
Mwanaspoti kuwa uongozi wa klabu yake ambao ulikutana juzi Jumanne, umefikia azimio la kutomwongezea Morocco mkataba baada ya ule wa awali kumalizika tangu Septemba 31.
“Kwa sasa timu itakuwa chini ya Ally Mohamed
‘Kidi’ na ndiye atakayeiongoza kwenda Kagera, mpaka hapo atakapopatikana
kocha mwingine, tunaangalia uwezekano wa kuchukua kocha kutoka nje ya
nchi,” alisema Kumwembe.
Alisema wamefikia uamuzi wa kutomwongezea mkataba
Morocco baada ya kutoridhishwa na viwango vya wachezaji wakati wanaamini
usajili waliofanya ni mzuri.
Mwanaspoti linajua kwamba kocha huyo amenyimwa
mkataba kutokana na staili yake ya kujilinda na kuogopa kushambulia
akihofia kupoteza mchezo. Uongozi umetafsiri staili hiyo kama kuishiwa
mbinu hasa kwa aina ya wachezaji waliosajiliwa.
No comments:
Post a Comment