Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, October 22, 2013

MBUNGE AWACHANA MAWAZIRI MBELE YA JK , WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA RAIS

a_7ea4a.jpg
Wananchi wa Mlangali wakiwa wamezuia msafara wa Rais Kikwete
b_80eef.jpg
Madai ya wana Ludewa kwa JK

c_2d981.jpg
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akisaidia kueleza kero za wana Ludewa kwa Rais Kikwete baada ya msafara wake kuzuiwa eneo la Mlangali leo
d_786a1.jpg
Msafara wa JK ukiwa umezuiwa eneo la Mbwila Ludewa leo
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe awafyatua mawaziri mbele ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wamekuwa wakitembelea jimbo lake la Ludewa wakati wa ziara ya Rais na waziri mkuu wakati siku zote wananchi wa jimbo hilo wanalia kwa kero mbali mbali.
Mbali ya kuwawasha mawaziri hao pia mbunge Filikunjombe amesema kuwa kero ya maji katika mji wa Ludewa ni kubwa na wananchi kwa zaidi ya wiki moja sasa hawana maji yamefungwa kwa ajili ya kuelekea Ikulu kwa matumizi ya Rais hali wananchi wa mji huo akiwemo yeye mwenyewe wamekosa maji ya kuoga kwa zaidi ya siku tatu sasa.
Mbunge Filikunjombe alitoa kauli hiyo leo katika uwanja wa Ludewa wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Kikwete.
Kwani alisema kuwa mbali ya jitihada mbali mbali ambazo serikali ya Kikwete imekuwa ikifanya katika kusukumba mbele maendeleo ya wana Ludewa kwa kuanza ujenzi wa lami , mradi mkubwa wa makaa ya mawe na mchuchuma ila bado wananchi hao hawana shaka na miradi hiyo isiyo kuwa wanataka miradi hiyo inanze kuwanufaisha wana Ludewa hata kwa ajira badara ya wageni kutoka Kenya kupewa vitalu katika migodi hiyo huku wakazi wa Ludewa wakipokonywa vitalu vyao.
Hata hivyo alisema kuwa ni vema miradi hiyo kuanza kwa kuwanufaisha wana Ludewa kwanza hata kwa ajira badala ya kuwatazama wageni kutoka Kenya ambao wamekuwa wakipewa vitalu katika miradi hiyo .
"Mheshimiwa Rais sisi Ludewa si kama Mtwara ambao walisema gesi haitatoka Mtwara ....sisi Liganga na mawe yatatoka kwenda mikoa mingine ila tunataka vijana wa Ludewa waanze kunufaika kwa ajira "
Pia mbunge huyo alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya mawaziri akiwemo waziri wa nishati ambae amekuwa akifikia wilaya ya Ludewa wakati wa ziara ya Rais badala ya kujenga utamaduni wa kuwatembelea wananchi mara kwa mara.
Alisema wananchi wa Ludewa wamekuwa na kero kubwa juu ya madini yao kwa wenyeji kupokonywa vitalu vyao na ofisi ya madini kanda nay eye kama mbunge amepata kufika ofisi ya waziri husika ila hakuna jibu la maana analolitoa kwake .
Hivyo kumwomba Rais Kikwete kuwabana mawaziri hao ikiwezekana ofisi ya madini kujengwa Ludewa na sio Mbeya kama ilivyo sasa.
Awali naibu waziri wa maji Dr Binilith Mahenge alimweleza Rais Kikwete kuwa wizara imetenga bajeti kwa ajili ya kufikisha maji katika vijiji mbali mbali vya wilaya ya Ludewa pamoja na eneo la mji wa Ludewa
Huku kwa upande wake naibu waziri wa nishati na madini George Simbachawene alisema kuwa wizara yake itaendelea kuwahudumia wananchi wa Ludewa na kuwaomba viongozi wa wilaya hiyo kuandaa ukumbi ili wataalam wake kuja kukutana na wananchi kwa ajili ya kupokea kero mbali mbali.
Wakati huo huo wananchi wa kata ya Madope na Mlangali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wamezuia msafara wa Rais Jakaya Kikwete kuomba kuharakisha ujenzi wa barabara ya lami kutoka Ludewa –Njombe pamoja na kero ya soko la mahindi ambayo wamedai yameendelea kuharibika katika nyumba zao
Wananchi hao wakiwa na mabango yanayoelezea kero hizo na nyingine walizuia msafara huo kwa nyakati tofauti wakati Rais Kikwete akitokea wilaya ya Njombe kuelekea makao makuu ya wilaya ya Ludewa kwa ajili ya ziara yake ya siku mbili wilayani Ludewa.
Kwa upande wao wananchi wa Madope ambako ni mpakani mwa wilaya ya Njombe na Ludewa walimwomba Rais Kikwete kusaidia kijiji hicho kupatiwa kituo cha afya pamoja
na kuomba umeme , mnara wa simu na barabara ya lami kutoka Njombe – Ludewa.
Wakati wananchi wananchi wa kata ya Mlangali wakimwomba Rais Kikwete kuwasaidia masoko ya mazao yao pamoja na kupatiwa huduma ya maji.
Akijibu kero za wananchi hao Rais Kikwete alisema kuwa serikali yake itaendelea kuwahudumia ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi zake.
Alisema kuhusu suala la mazao kukosa soko alisema kwa sasa serikali imenunua mazao kiasi cha kutosha na kuwa tayari imewataka watu binafsi kujitokeza kununua mazao hao.
Pia alisema suala la barabara tayari barabara ya Ludewa – Njombe ipo katika mkakati wa kujengwa kwa kiwango cha lami na tayari ujenzi huo umeanza katika mji wa Ludewa.
Kuhusu suala la maji alisema kuwa kwa kawaida upo usemi usemao kuwa wageni njoo wenyeji tupone ila ameshangazwa kuona Ludewa ni tofauti wageni wanapokuja ndipo wananchi wanapata kero ya maji.
" Ila mimi sikupenda ninapokuja ninyi mkose maji ....mimi nitaondoka kesho tu ila upo mkakati wa serikali wa kutatua kero ya maji mijini na ninawaahidi katika kipindi kifupi kero hii ya maji itamalizika tayari bajeti ipo na shabaha yetu kutatua kero hiyo"
Akielezea kuhusu suala la umeme alisema vijiji zaidi ya 74 vitanufaika na umeme vijijini vikiwemo vijiji vya Mlangali , Madope na vijiji vingine vyote vya njiani kuelekea Songea na tayari mkandarasi amepatikana na kuwataka wananchi kuanza mandalizi ya kuingiza umeme.
Hata hivyo Rais Kikwete akielezea kuhusu ujenzi wa barabara ya lami alisema kuwa kazi hiyo ina kazi zaidi ya moja ikiwemo ya uchoraji ramani na upembuzi yakinifu zoezi ambalo linaendelea kabla ya zoezi la tatu kuanza.
Alisema kuwa kwa upande wa Ludewa tayari Km mbili na nusu zimekwisha jengwa na sasa wasubiri kuanza ujenzi wa barabara yote ya Ludewa - NJombe .
Kuhusu ahadi ya meli ambayo mbunge Filikunjombe alimtaka Rais kutolea ufafanuzi alisema kuwa serikali ipo katika mchakato wa kutekeleza ahadi hiyo.
Alisema kuwa serikali itanunua meli tatu kwa ajili ya maziwa matatu Tanganyika , Nyasa na Victoria na kuwa tayari kupata meli zinafanyika na nchi zaidi ya mbili zinataka kuleta meli hivyo kuwa na meli mbili kila ziwa
Rais Kikwete alimtaka mbunge Filikunjombe kuendelea kufuatilia suala hilo kwa waziri DR Mwakyembe ili kuona ahadi hiyo inatekelezeka.

No comments:

Post a Comment