| Rais Kikwete akizungumza na viongozi wa mkoa wa Njombe katika majumuisho ya ziara yake mkoa wa Njombe |
| Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga akimpongeza mkuu wa mkoa wa Njombe Aser Msangi kulia kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuendeleza mkoa wa Njombe |
| Viongozi wa mkoa wa Njombe wakisubiri kumpokea Rais Kikwete katika ukumbi wa Halmashauri |
| Rais Kikwete akisikiliza kwa makini maelezo ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe |
........................................................................................................
Rais Jakaya Kikwete amehitimisha ziara yake
mkoani Njombe kwa kupongeza
jitihada kubwa za maendeleo
ambazo zimeendelea kuonekana
katika mkoa huo.
Mbali ya kupongeza jitihada hizo pia alisema kuwa
serikali yake itaendelea kuwa
karibu na wananchi wa mkoa
wa Njombe na watanzania kwa ujumla
na kuwa sehemu
kubwa ambayo amepata kupita
katika wilaya za
mkoa wa Njombe wananchi
wanalalamikia soko la mahindi
na kuendelea kudai
fedha zao kwa wakala wa mazao
ya chakula.
Rais Kikwete
ametoa pongezi hizo leo
katika ukumbi wa Halmashauri
ya wilaya ya Njombe wakati
wa majumuisho ya ziara yake siku
sita katika mkoa
wa Njombe
Alisema kuwa
tayari mchakato wa kuwalipa wakulima madeni
yao ya mahindi waliouza kwa wakala
wa chakula na amepata kuwasiliana
na waziri wa fedha
Dr Wiliam Mgimwa ili
kuona wakulima hao wanmalipwa fedha zao.
Aidha amesema kumekuwepo na maombi ya wakulima
kuwa wana mahindi ambayo yamekosa
soko na kuiomba serikali kununua mazao
hayo japo ni wazi serikali imekuwa ikinunua mahindi kwa ajili
ya akiba na tayari zoezi hilo la kununua mahindi kwa akiba limekamilika.
Alisema kuwa hadi sasa
tayari tani zaidi ya 4000
zimenunuliwa nab ado tani 49000 hivyo
wakati wakiendelea na zoezi hilo atawashauri kwenda
kununua mahindi hayo ambapo hata
hivyo tani zaidi ya 300,000 za
mahindi ya wakulima wa mkoa
wa Njombe hazitanunuliwa na serikali hivyo kuwataka
viongozi wa mkoa wa Njombe
kutafuta soko kwa watu
binafsi.
Hata hivyo alisema
kuwa awali serikali iliweka vizuizi
barabarani kuzuia mahindi kutoka
nje ila
baada ya uchunguzi
imebainika kuwa zoezi hilo linawanufaisha wale
weanaokaa katika vizuizi huku mahindi
yakiendelea kupita .
Pia rais Kikwete aliwahakikishia wakulima
kuwa serikali kwa mwakani imejipanga kuanza
kununua mahindi mapema
zaidi na kuwa haitaweka akiba ya
mchele katika maghala ya
Taifa isipo kuwa kwa mkoa wa Dodoma watanunua
mtama kama akiba
Hata hivyo rais Kikwete
amepongeza jitihada za kuendeleza
zao la pareto katika mkoa huo na kupiga
marufuku wale wote wanaonunua pareto moja kwa moja kutoka kwa wakulima
huku wakikwepa kodi .
Alitaka viongozi wa
Halmashauri ya Makete na mkoa kuwabana
watu hao wanaokwenda kulipa kodi na kutaka ofisi zinazotoa vibali kuweka masharti ya watu hao
wanaopewa vibali vya kununua
zao la pareto kuripoti ofisi za Halmashauri ili kulipa kodi.
Kwani alisema
hakuna serikali inayoendeshwa bila kodi
hivyo ni wajibu wa
kila mmoja kulipa kodi hiyo kupitia zao hilo la Pareto.
Alisema ni vema
Halmashauri kubuni mbinu nzuri ya
kukusanya mapato yasiyo na usumbufu badala ya
kuendelea kuwabana mamalishe
ambao wanafanya shughuli
hizo kwa ajili ya kijikimu .
Kuhusu
uendelezaji wa mazao mengine ya
biashara aliwataka viongozi
wa mkoa wa Njombe kubuni mbinu
nyingine ya kubuni mazao ya biashara
kama kilimo cha miti ,maua na mazao mengine ya biashara ili
kukuza uchumi wa wakazi
wa Njombe.
“ Msipuuze
kilimo cha matunda ,nyanya na mboga
mboga kwani ni kilimo ambacho
kina faida kubwa
na kinaweza kumwezesha mwananchi
kukuza uchumi wake…muwe na mpango wa
kuendeleza kilimo cha matunda
badala ya kutegemea matunda
kutoka Afrika ya kusini na sasa
watanzania wanakula sana matunda “alisema Rais
Kikwete
Alishauri wilaya
ya mikoa
kuwatumia mabwana shamba wake
katika kufundisha wananchi
kulima mazao mapya ya biashara
ikiwa ni pamoja na kutumia chuo
cha Kilimo Uyole kwa ajili ya kuwapa mafunzo hasa
wale mabwana shamba
wanaofundishika .
Kwani alisema kuwa maeneo yote dunia ambayo hayana mazao ya biashara wananchi wake wamekuwa wakiongoza kwa umasikini.
Alisema kuwa moja kati ya mazao ambayo
ni vigumu kupandisha bei ni pamoja na mazao ya chakula ila mazao
ya biashara mtu anaweza kuongeza bei .
" Natumaini wananchi wetu iwapo
watalima mazao ya biashara wataweza kujikwamua zaidi kiuchumi badala
ya kubaki wakilima mahindi pekee ambayo yatamfanya kuendelea kuwa
masikini.....sisi kama serikali tutaendelea kuwaunga mkono wananchi
ambao wanaendesha pia mazao ya biashara "
Rais Kikwete alisema kuwa mbali ya
ziara hiyo bado atafika tena katika mkoa wa Njombe ili kutembelea
maeneo yanayolima matunda na mazao mengine ya biashara kama maua na
mengine.chanzo Francis Godwin

No comments:
Post a Comment