Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitoa salamu za mwisho kwa mwili
wa hayati Meja Anthony Igobeko aliyefariki Oktoba 18 baada ya kuugua
kiharus. Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilifanyika jana kwenye kambi
ya jeshi Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma na baadae mwili
ulipelekwa Dar es salaam kwa maziko.
Mkuu
wa Jeshi kanda ya Dodoma Brigadia Masumbuko Mdeme akitoa salamu za
mwisho kwa Mwili wa hayati Meja Anthony Igobeko aliyefariki Oktoba 18
baada ya kupata kiharusi. Ibada ya kuuaga mwili wa mareheu ilifanyika
jana kwenye kambi ya jeshi Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma na baadae
mwili ulipelekwa Dar es sallaam kwa maziko.
Mwili
wa marehemu Meja Anthony Igobeko ukiwa umebebwa kwenda kupakiwa kwenye
gari tayari kuusafirisha kwenda Dar es salaam kwa mazishi, kushoto ni
Mkuu wa Jeshi kanda ya Dodoma Brigadia Masumbuko Mdeme na Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi wakishuhudia.
Baadhi
ya Ndugu wa karibu wa Hayati Meja Anthony Igobeko waliohudhuria Ibada
ya kumuaga iliyofa nyika jana kwenye Kambi ya Jeshi ya Ihumwa iliyopo
nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
Baadhi ya wapiganaji wa Jeshi la Wananchi JWTZ kanda ya Dodoma waliojitokeza kuuaga Mwiliwa Marehemu Meja Igobeko.
.................................................................................................
.................................................................................................
Mkuu
wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi mwishoni mwa wiki aliwaongoza
mamia ya maafisa ngazi za juu,chini na wapiganaji waJeshi la Wananchi
JWTZ kuuaga mwili wa aliyekuwa mmoja kati ya wakuu wa vikosi vya Jeshi
Mkoani Dodoma hayati Meja Anthony Igobeko aliyefariki Oktoba 18 kufuatia
kuugua kiharusi.
Ibada
ya kuuaga Mwili wa Hayati Meja Igobeko tayari kwa kuusafirisha kuelekea
Dar es salaam ilifanyika jana kwenye kambi ya Jeshi Ihumwa nje kidogo
ya Mji wa Dodoma. Kwa upande wake Kapteni Manyiga wakati akitoa taarifa
kwa umma uliokusanyika kumuaga hayati Meja Igobeko, alisema kuwa Meja
Igobeko hakuwa katika hali ya kuugua wala kusumbuliwa kiafya isipokuwa
Oktoba 18 asubuhi alipata kiharusi na kufariki majira ya mchana.
Akimuelezea
hayati Meja Igobeko , Mkuu wa Jeshi kanda ya Dooma Brigadia Masumbuko
Mdeme alisema kuwa Meja Igobeko alikuwa Mpiganaji Mahiri, Afisa Mkuu
Mwadilifu, mtiifu na hodari,alikuwa mwepesi kutekeleza amri; kwa ujumla
alikuwa na sifa za kiongozi na kuwa Jeshi limepata limepata pigo.
Akitoa
salamu za Mkoa Mkuu wa Mkoa wa DodomaDr. Rehema Nchimbi alisema kuwa
majonzi hayaendi kwa wanandugu pekee bali ni kwa mkao mzima wa Jeshi.
Amelitaka jeshi kuikabili hali hiyo akionesha imani kubwa aliyonayo kwa
jeshi-JWTZ, aidha amelitaka Jeshi kuendelea kujipanga na kuongeza
ufanisi.
Akiwaasa
mamia yawapiganaji waliokusanyika Kambini hapo kuuaga mwili wa
mpiganaji mwenzao, amewataka wote kumuenzi Hayati Meja Igobeko kwa
kuishi na kufanya yale mazuri ya mfano aliyoyafanya Meja Igobeko enzi za
Uhai wake.
Akitoa
salamu za familia, mwakilishi wa familia ya marehemu Igobeko Ndg.
Emmanuel Masaga alilishukuru Jeshi kwa kumlea ndugu yao na kumuhangaikia
sana wakati alipopata kiharusi na kusema kuwa hiyo inaonesha kuna
ushirikiano mkubwa na upendo katika jeshi la wananchi wa TAnzania.
Akitoa
wasifu wa Marehemu Meja Igobeko, Kapteni Manyiga alisema kuwa marehamu
alizaliwa mwaka 1959 mkoani Mwanza, alijiunga na jeshi mwaka 1980 na
alikuwa wa mfano Jeshini, alikuwa na ustawi mzuri hadi kufikia ngazi ya
Meja mwaka 1995. Vilevile alishatunukiwa nishani mbalimbali zikiwemo
miaka 40 ya Jeshi la Wananchi JWTZ, utumishi wa muda mrefu na utumishi
uliotukuka. Aliongeza kuwa marehemu ameacha mke na watoto 4.
No comments:
Post a Comment