MECHI baina ya Mbeya City na Prisons imeingiza Sh 31.6 milioni huku watu sita wa jijini Mbeya wakikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwapiga mawe wachezaji wa Prisons na kuvunja vioo vya magari juzi Jumanne.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Robert
Mayala, alisema mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo baadhi ya vijana
walijikusanya nje ya uwanja huo eneo la Rift Valley na kufanya vurugu
hizo.
“Mpira ulimaliza kwa amani kabisa, lakini
mashabiki wakiwa wanatoka uwanjani kuna kundi la vijana walikuwa
wamejikusanya eneo la Rift Valley na kulishambulia basi la wachezaji wa
Prisons na kuwajeruhi baadhi ya wachezaji pamoja na kuvunja vioo,”
alisema Mayala.
Aliwataja waliokamatwa na kufikishwa mahakamani
kuwa ni Enock Jeremeiya, David Daniel, Emmanuel Ndalu, Michael George,
David Laurent na Vicent Ramadhan.
Awali, Katibu Mkuu wa Tanzania Prisons, Sadick
Jumbe, alilaani kitendo cha kushambuliwa kwao na kubainisha kwamba
vurugu hizo ni dhahiri kuwa hazilengi kujenga umoja na mshikamano kwa
wakazi wa jiji hilo na vitongoji vyake.
Katika hatua nyingine, mchezo huo uliingiza
mashabiki 10,558. Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya,
Suleiman Haroub, alisema kutokana na mapato hayo kila timu ilipata
asilimia 29.5 sawa na Sh 6, 987,000.CHANZO MWANASPOTI
No comments:
Post a Comment