Meneja
Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) Bw. David Mziray akitoa wito kwa wamiliki wa Pikipiki na
madereva wa usafiri huo kushirikiana katika kuhakikisha wanatekeleza
sheria na kanuni zilizowekwa na Mamlaka hiyo, wakati wa Mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Udhibiti wa Usafiri Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Gilliard Ngewe akieleza kwa waandishi wa
Habari(hawapo pichani) juu ya Kanuni za Kudhibiti Usafiri wa Pikipiki na
Bajaj, wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)
leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari
Bi.Fatma Salum.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imewataka wamiliki na madereva wa pikipiki na Bajaji kufuaata na kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa barabara Gilliard
Ngewe wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam.
Ngewe
amewataka wamiliki na waendesha vyombo hivi kuzingatia wajibu wao kwa
kujiwekea mfumo wa udhibiti wa ndani wa kuhakikisha wanaheshimu sheria,
na kudhibiti vitendo vyote vya uvunjaji wa sheria na kulinda usalama
wao na abiria wao.
Aliongeza
kuwa ni vyema wamiliki wakatambua masharti ya Leseni zao ambayo
aliyataja kuwa ni kwanza pikipiki husika kutoa huduma katika eneo
lililoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na lazima pikipiki husika zikidhi
viwango vya shirika la viwango.
Alifafanua
zaidi kuwa dereva wa pikipiki haruhuswii kubeba abiria zaidi ya mmoja
ambapo kwa pikipiki za miguu mitatu zinatakiwa kubeba abiria kama
inavyotakiwa kwa mujibu wa leseni zao zinazowapa kibali cha kubeba
abiria wasiozidi watatu.
Pia
Dereva wa pikipiki anatakiwa kuvaa kofia ya kujikinga na kuwa na alama
ya eneo analofanyia biashara ya kubeba abiria. Ngewe alisema
Ngewe aliongeza kuwa abiria wanatakiwa kuvaa kofia ya kujikinga wakati wote wanapotumia usafiri wa
huo ili kuepusha madhara yanayoweza kuwapata mara ajali inapotokea.
Naye
Meneja mawasiliano wa Mamlaka hiyo David Mziray alisema wanashirikiana
na mamlaka nyingine kama halmashauri za miji na polisi katika
kuhakikisha kuwa sheria na kanuni za usafirishaji zilizowekwa
zinazingatiwa.
Sumatra
imewataka wamiliki na waendeshaji wa vyombo hivi kujiwekea mfumo wa
udhibiti wa ndani na kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya kihuni na
kulinda usalama wao wenyewe na abiria.
No comments:
Post a Comment