MSAFARA WA WAZIRI NCHIMBI HAUKUPIGWA MAWE SONGEA
Habari
iliyotolewa Oktoba 26, mwaka huu na baadhi ya magazeti na mitandao ya
kijamii yenye kichwa cha habari 'Msafara wa Waziri Nchimbi wapigwa mawe
Songea' si za kweli bali zimetengenezwa na walizituma kwa nia ya
kupotosha jamii.
Oktoba 25,
mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Songea
Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi alitembelea Miradi ya Maendeleo pamoja na
kufanya Mkutano aliianza katika Kata ya Mletele na kumalizia Kata ya
Matarawe, katika jimbo lake la Songea Mjini. Wakati alipomaliza mkutano
wake wa Mletele alitaarifiwa makundi ya watu yamefunga njia katika
daraja la Matarawe na wamesema hawatalifungua mpaka Mhe Nchimbi
akaliangalie na kuzungumza nao.
Mhe.
Nchimbi alishauriwa kubadili njia ili kuwahi mkutano wa hadhara wa
Matarawe ambapo wananchi walikuwa wanamsubiri kwa zaidi ya saa mbili.
Pamoja na kushauriwa kupita njia nyingine, Mhe. Nchimbi aliamua kwenda
kuwasikiliza, alifika katika eneo la daraja akiwa amefuatana na viongozi
mbalimbali wa Manispaa na Serikali, mhe Nchimbi aliwapa fursa wananchi
hao kueleza kero zao, nao walimwambia kuwa eneo hilo limekuwa na ajali
mara kwa mara tokea barabara ya lami ilipokamilika na kusababisha vifio
vya watu karibu wanne hivyo walimuomba mbunge wao awasaidie kumaliza
kero hiyo.
Akijibu
kero hiyo, Mhe. Nchimbi aliwaambia wananchi wake kuwa ni yeye
aliyefanikisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami
atalishughukia tatizo hilo pia na kuwa amelichukua kwa uzito mkubwa.
Baada ya majibu ya mhe Nchimbi wananchi hao waliridhika na ndipo wenyewe
wakafungua barabara na kutoa vizuizi ili waziri na msafara wake waweze
kupita. Mhe Nchimbi na ujumbe wake waliendelea na safari na kwenda
kwenye mkutano wa hadahara takribani mita 200 toka daraja hilo. Saa moja
baada ya mhe Nchimbi kuwa ameshapita baadhi ya vijana walifunga tena
barabara na ndipo Jeshi la Polisi lilipolazimika kuwatawanya na kuwakama
vijana saba.
Waandishi
wa habari wa Televisheni za Star TV, Channel Ten na TBC wanamikanda ya
tukio zima na hivyo mikanda hiyo inaweza kuthibitisha habari kuwa mhe
Nchimbi alipigwa mawe ni uzushi mtupu.
Waziri
Nchimbi alikuwa katika ziara ya kawaida jimboni kwake na aliweza kufanya
mikutano minane ya hadhara iliyohudhuriwa na mamia ya watu na
iliendeshwa kwa utulivu mkubwa ambapo wenyeviti wa mikutano hiyo
walikuwa madiwani wa kata husika, ambapo katika kata sita mikutano hiyo
iliongozwa na madiwani wa CCM na kata mbili iliongozwa na madiwani wa
Chadema.
Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi inavisihi vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii kujiridhisha na ukweli wa taarifa wanazozipata kabla ya kuzitoa
kwa wananchi ili wananchi waweze kupata haki yao ya kupata habari
zilizokuwa sahihi.
Mwisho.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
28 Oktoba, 2013
No comments:
Post a Comment