Katika
Gazeti la Mawio Toleo Namba 0062 la tarehe 26.9.2013 – 02.10.2013 na
toleo Namba 0063 la tarehe 03.10.2013 zimechapishwa habari zenye vichwa
vya habari "Mtandao wa Ujangili Huu Hapa" na "Wabunge CCM watajwa
ujangili".
Katika habari zote hizo zimelihusisa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama chanzo cha habari hizo.
Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusiana na taarifa hizi:
(i)
Shirika la Hifadhi za Taifa halijawahi kudhamini ripoti iliyotajwa
katika habari hizo kuhusiana na utafiti makini wa ujangili.
(ii) Shirika husimamia shughuli za uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi
za Taifa pekee kiutendaji, ambapo baadhi ya maeneo yaliyotajwa
Katika habari hizo kama Selous na Liwale kiutendaji hayapo ndani
ya Shirika la Hifadhi za Taifa.
(iii)
Kama Shirika la Umma, hufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na
kushirikisha vyombo mbalimbali vya dola katika kushughulikia uhalifu wa
aina mbalimbali ikiwemo ujangili.
Ni kwa
mantiki hii basi, shirika linapenda kuweka bayana kuwa halihusiki na
taarifa hizo, na hata pale zinapopokelewa zina utaratibu wake wa
kufanyia kazi.
Tunachukua
nafasi hii kuviomba vyombo vya habari kushiriki katika juhudi za
kupambana na ujangili kwa kuwa waangalifu katika kuandika habari za
kutuhumiana kabla ya kuwa na ushahidi kamili ambao ni haki ya kimsingi
ya kisheria inayopaswa kuheshimiwa.
Imetolewa na Idara ya Uhusiano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
No comments:
Post a Comment