Zanzibar. Waraka wenye vitisho ukiwa na nembo ya Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) umesambazwa visiwani hapa, ukidaiwa kutishia kufanyika kwa shambulio dhidi ya viongozi wa dini na Serikali kabla ya Sikukuu ya Eid El Haj.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,
Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha kupata nakala ya waraka huo wenye
maneno makali na vitisho kwa usalama wa watu na amani ya nchi. Kamanda
Mkadam alisema,Polisi imefanikiwa kuupata waraka huo baada ya tukio hilo
kuripotiwa na baadhi ya viongozi wa madhehebu za dini Visiwani humo.
Hata hivyo, alisema,tayari makachero wa Polisi
wako kazini na ametoa wito kwa viongozi wa dini na wananchi kuondoa hofu
kwa vile vyombo hivyo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kukabiliana na
tukio lolote la kihalifu.
Aliwahi wananchi kuendelea na jitihada za kuwafichua wahalifu na watu wanaowatilia shaka dhidi ya amani visiwani hapa.
“Hatua tulizochukua ni pamoja na kuwataka viongozi
wa dini kuanzisha kamati za ulinzi mbali na kuwapatia huduma za ulinzi
kama njia ya kukabiliana na matukio mbalimbali,”alisema Kamanda Mkadam.
Waraka huo unadaiwa kuainisha vitendo vya hujuma
kuwa vitazidi hadi pale Zanzibar itakapofanikiwa kurejesha kile
kilichoitwa Uhuru wake.CHANZO GAZETI LA MWANAINCHI
No comments:
Post a Comment