WATU
saba wamekufa papo hapo kwenye ajali mbaya iliyotoka leo alfajiri katika
kijiji cha Dakawa - Sokoine Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Ajali
hiyo iliyohusisha gari ya abiria aina ya Noah yenye namba za usajili T
502 AUP iliyokuwa ikitoka Wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro mjini
kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129
AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora.
Watu
saba wamepoteza maisha katika ajali huyo akiwemo dereva wa Noah
aliyejulikana kwa jina la Masoud Juma na wengine wanne hali zao ni
mbaya. "Chanzo cha ajali hii ni dereva wa Noah ambaye alikuwa akijaribu
kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla akakutana na lori uso kwa
uso" Alisema Bw. Sanjo Ole ambaye ni mfugaji jamii ya Kimasai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo.(HABARI NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)

No comments:
Post a Comment