Mwenyekiti
wa MeTL Group Bw. Gulam Dewji akibadilishana mawazo na aliyekuwa Rais
wa Botswana Mh. Festus Gontebanye Mogae alipomtembelea rafiki yake
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group ambaye pia ni Mbunge wa
Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) ofisini kwake.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group Mh. Mohammed Dewji siku ya
jana alipata nafasi ya kuzungumza na rafiki yake, aliyekuwa Rais wa
Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae. Mh. Mogae ambaye
pia amewahi kuwa mshindi wa tuzo ya Mafanikio katika Uongozi itolewayo
na mfanyabiashara mzawa wa Sudan Bwana Mo Ibrahim mwaka 2008, alikuwa na
mazungumzo binafsi na Mohammed Dewji (Mo) alipomtembelea ofisini kwake
jijini Dar-es-salaam.
Tuzo
hiyo ya Mo Ibrahim, humuwezesha mshindi kupata kitita cha dola za
Kimarekani millioni 5, na dola za Kimarekani 200,000 kila mwaka kwa
maisha yake yote. Hizi ni baadhi ya picha, zilizopigwa na mpiga picha
wetu, jana kwenye ofisi za MeTL Dar-es-salaam.
Mh.
Mohammed Dewji katika picha ya pamoja na aliyekuwa Rais wa Botswana
(1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae.
No comments:
Post a Comment