Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi.
Na Khatimu NahekaMSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi amesema ataendelea kujituma katika kikosi hicho, lakini kwa mara ya kwanza akazungumzia juu ya muda ambao ataihama timu hiyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Bahanuzi ambaye ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, alisema hana wasiwasi juu ya uwezo wake, lakini kama ataendelea kukosa nafasi, ataikimbia klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Bahanuzi ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora katika timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Kagame misimu miwili iliyopita, amesema hawezi kuvumilia kukaa nje wakati anaamini bado uwezo wa kuitumikia Yanga anao.
“Kazi yangu ni mpira, ili niendelee kutumia kipaji changu, natakiwa kucheza katika mechi, nafurahi kuwa hapa lakini sifurahii kuwa nje, naamini uwezo wangu, nitavumilia kwa kujituma zaidi mazoezini, ikitokea hali ikazidi kuendelea, nafikiri naweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu,” alisema Bahanuzi aliyetua Yanga akitokea Mtibwa Sugar.
No comments:
Post a Comment