Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 3, 2013

BALE, RONALDO Waiongoza MADRID kuibamiza rayo vallecano 3-2


bale 9c5fb
WINGA Gareth Bale amewathibitishia mashaiki wa Real Madrid kwamba yeye ni mkali na guu la kushoto, baada ya jana kutoa pasi za mabao mawili katika ushindi wa 3-2 wa timu hiyo dhidi ya Rayo Vallecano.

Wakiwa wanaitwa Mabao ya Euro Milioni 194 mjini Madrid – Ronaldo alimalizia pasi ya Bale na kama ilivyokuwa katika ushindi wa 7-3 dhidi ya Sevilla kawikati ya wiki, wawili hao wishirikiana katika bao la tatu.
Bale alimtoka Anaitz Arbilla upande wa kulia kabla ya kumtilia krosi Ronaldo ambaye alifunga bao lake la 13 msimu huu.
Real Madrid waliongoza kwa 3-0, Ronaldo akifunga la kwanza dakika ya tatu na la pili dakika ya 48 kabla ya Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya 31, lakini wapinzani wao walikuja juu kipindi cha pili na kujpata bao la kwza dakika ya 53 kwa penalti mfungaji Viera ambaye alifunga tena dakika ya 55.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Diego Lopez, Carvajal/Arbeloa dk59, Pepe, Sergio Ramos, Coentrao/Marcelo dk45, Xabi Alonso/Illaramendi dk45, Modric, Bale, Di Maria, Ronaldo na Benzema.
Rayo Vallecano: Ruben; Tito, Galvez, Arbilla/Larrivey dk51, Nacho; Adrian, Saul; Trashorras, Lass, Falque/Embarba dk69 na Viera. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment