Dkt. Sengondo Mvungi, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi ambaye pia ni Mjumbe
wa tume ya Katiba (pichani), amevamiwa usiku wa kuamkia leo nyumbani
kwake jijini Dar es salaam na amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa katwa na
mapanga na watu wasiofahamika ambao habari za awali zinadai kuwa ni
majambazi.
Akithibitisha tukio
hilo, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mahusiano ya Umma wa
NCCR-Mageuzi Taifa, Mhe Moses Machali, ameiambia Globu ya Jamii muda
mfupi uliopita kwamba Dkt Mvungi alijeruhiwa vibaya sana usiku (wa
kuamkia leo) saa 6.Mhe Machali
amesema taarifa zilizopatikana ni kwamba walimkata mapanga
hasa kichwani na kumsababishia kupoteza fahamu, na kwa sasa yupo
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
"Wana NCCR-Mageuzi na Watanzania wote tupeane pole kwa uvamizi wa Dkt Mvungi. Tumwombee na kumtakia apate kupona haraka", alisema Mhe. Machali, ambaye pia ni Mbunge wa Kasulu Mjini, akiongezea kuwa hali yake ni mbaya.
No comments:
Post a Comment