Wafuasi wa CUF wakiingia Donge na kubeba ujumbe wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Wafuasi wa CUF wakiwa wakibeba ujumbe mzito katika eneo la Donge.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muwanda Jimbo la Donge.
Vijana wa CUF Donge, wakighani utenzi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Muwanda Donge.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akipandisha bendera katika moja ya matawi mapya ya chama hicho katika eneo la Donge.
Wafuasi wa CUF wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi kadi kwa mmoja wa
wanachama wapya waliojiunga na chama hicho katika Jimbo la Donge.
Wafuasi wa CUF wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Picha na Salmin Said, OMKR
Na Hassan Hamad, OMKR
Hatimaye
Chama Cha Wananchi (CUF) kimeingia katika kijiji cha Donge kufanya
mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muwanda na kuhutubiwa na Katibu
Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Maelfu ya
wafuasi wa Chama hicho kutoka maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini
walijitokeza katika mkutano huo ili kushuhudia kile kilichokosekana kwa
muda mrefu kuingia katika eneo hilo la Donge kwa ajili ya Mkutano wa
hadhara.
Akizungumza katika
mkutano huo, Maalim Seif amesema anajisikia fahari kuzungumza na
wananchi wa Donge katika eneo la ndani la jimbo hilo.
Amesema
Donge ni kijiji chenye historia ndefu na ambacho kimejipatia umaarufu
mkubwa Zanzibar baada ya kutoa wanazuoni kadhaa, pamoja na kutajwa kwao
kushiriki kikamilifu katika Mapinduzi ya mwaka 1964.
Kuhusu
mamlaka kamili amesema suala hilo limeanza kudaiwa tangu wakati wa
marehemu mzee Karume, na kwamba wanaobeza kudai mamlaka ya Zanzibar
wanabeza kauli za Mzee Karume ambapo katika mkutano huo pia iliwekwa
sauti ya Mzee Karume alipokuwa akitaja malengo ya Mapinduzi.
Maalim
Seif aliingia Donge mapema asubuhi ambapo kabla ya mkutano huo alifanya
shughuli za kuimarisha chama ikiwa ni pamoja na kufungua matawi ya Chama
hicho, barza pamoja na kuweka jiwe la msingi katika tawi la CUF Donge
Muwanda.
Katika
Mkutano huo Maalim Seif pia alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 234,
baadhi yao wakiwa wanachama na viongozi waliokihama Chama cha Mapinduzi
kwa sababu tofauti, mmoja wao nd. Salim Khamis Nassor akiwa mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa Wilaya (CCM).
No comments:
Post a Comment