Askari polisi wakiwa na silaha wakiwa wamezingira nyumba iliyokuwa ikitumika kwa shughuli za kutolea Mimba.
Daktari mstaafu wa hosptali ya rufaa ya Mawenzi Frances Shayo akiwa mikononi mwa polisi muda mfupi baada ya kumkamata akitaka kuwatoa mimba wasichana wawili.
Mmiliki wa nyumba iliyoko kata ya Nga'mbo katika manispaa ya Moshi aliyefahamika kwa jina moja la Minde akipokea kichapo toka kwa askari polisi baada ya kukaidi kuingia kwenye gari la polisi.
Mmoja wa wanawake waliokutwa katika nyumba hiyo wakidaiwa
kumsindikiza binti mmoja ambaye ni mwanafunzi kwenda kwa daktari huyo
kutoa ujauzito.
Msichana Irene Musa ambaye anadaiwa kuwa mwanafunzi wa shule ya
sekondari Komkwa Masama wilayani Hai akitolewa kwenye nyumba ambayo anadaiwa kwenda kutolewa ujauzito .
Mmoja wa wanawake waliokutwa katika nyumba hiyo akidaiwa kwenda kutoa ujauzito kwa daktari huyo.
Umati wa watu waliofika katika nyumba ambayo inadaiwa kufanyika vitendo vya kutoa mimba. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kumnasa daktari mstaafu
wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi,mkoani Kilimanjaro, Frances Shayo(56)
akiwa katika harakati za kuwatoa mimba wanawake wawili akiwemo Irene
Musa(18) mwanafunzi wa shule ya sekondari Nkwereko iliyoko Masama
wilayani Hai.
Daktari huyo ambaye anatajwa kufanya vitendo hivyo
mara kwa mara amekamatwa pamoja na watu wengine watano wakiwa katika
nyumba ya mkazi wa Kata ya Ng’ambo aliyefahamika kwa jina moja na
Minde.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema daktari
huyo amekuwa akifanya shughuli hiyo kwa muda mrefu katika eneo hilo na
mara nyingine amekuwa akifanya shughuli za kuwatairi watoto katika
nyumba ya rafiki yake huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari
daktari Shayo amesema msichana huyo alifika katika nyumba hiyo akiwa na
tatizo la kufunga kutokwa na damu hivyo alikuwa kwenye harakati za
kutaka kumsaidia .
Kwa upande wake mama mzazi wa binti huyo,Rozi
Urasa amesema alifika nyumbani kwa daktari huyo baada ya kushauliwa na
baadhi ya ndugu zake kumpeleka kutoa ujauzito huo kutokana na kwamba
huenda binti huyo akakosa kazi pindi atakapokuwa akitafuta kazi akiwa na
ujauzito.
No comments:
Post a Comment