Kiongozi wa waasi wa LRA Joseph Kony ataka kuhakikishiwa usalama wake ili ajisalimishe
Serikali
ya Jamuhuri ya Afrika ya kati CAR imesema inajadiliana na kiongozi wa
waasi na raia wa Uganda Joseph Kony mwenye lengo la kujisalimisha.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya jamuhuri ya kati,Joseph Kony ametaka kuhkikishiwa usalama wake kabla hajajisalimisha.
Kony,ambaye ni kiongozi wa waasi wa LRA anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita anakokabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita.
Serikali ya Marekani iliahidi kutoa kitita cha dola za Marekani milioni 5 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa Joseph Kony.
Hii ni kwa mara ya kwanza Joseph Kony anapatikana tangu miaka kadhaa kupita.
Siku ya
jumatano mjumbe maalumu wa umoja wa Afrika Francisco Madeira,
alibainisha kuwa baraza la usalama la umoja wa mataifa limeona ripoti
kuwa Joseph Kony anaugua sana ugonjwa ambao haujaweza kufahamika.
Mnamo
mwezi April Jeshi la Uganda lilisitisha harakati za kumsaka Kony huko
jamuhuri ya Afrika ya kati wakilaumu kufanyiwa ukatili na serikali ya
waasi iliyokuwa ikidhibiti huko.
Joseph
Kony na wapiganaji wanaokadiriwa kufikia 200-500 wa kundi la waasi wa
Lord's Resistance Army (LRA) limesababisha mapigano nchini Uganda na
ukanda huo kwa zaidi ya miongo miwili.
No comments:
Post a Comment