Mfadhili
wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Orphan Program(IOP) la Iringa,
Yokes na Klaas wakimkabidhi moja ya vifaa mganga mkuu wa hospitali ya
Ilula Dk. Erasto Rite alivyoikabidhi hospitali teule ya Ilula
makabidhiano yaliyofanyika katika hospitali hiyo ilula
iliyoko
wilaya ya Kilolo mkoani Iringa2. Mfadhili wa shirika lisilo la
kiserikali la Ilula Orphan Program(IOP) la Iringa, Klaas akionyesha moja
ya vifaa vya kuongeza joto kwa watoto alivyoikabidhi hospitali teule ya
Ilula makabidhiano yaliyofanyika katika hospitali hiyo ilula iliyoko
wilaya ya Kilolo mkoani Iringa3. Mfadhili wa shirika lisilo la
kiserikali la Ilula Orphan Program(IOP) la Iringa, Klaas akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Ilula na
wafanyakazi wa IOP. (Picha zote na Denis Mlowe)
========= ======= ==========
HOSPITALI TEULE YA ILULA YAPATIWA MSAADA
Na Denis Mlowe,Ilula
MFADHILI
wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Orphan Program(IOP) la Iringa,
Yoker n Klaas ametoa msaada wa vifaa tiba na ukarabati wa majengo ya
hospitali teule ya Ilula iliyoko katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 32 kwa ajili ya kuwasaidia
mama wajawazito na watoto wanaozaliwa kabla ya muda(njiti).
Akizungumza
wakati akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa mganga mkuu wa hospitali
hiyo Dk. Erasto Rite katika makabidhiano yaliyofanyika katika hospitali
hiyo, Klaas alisema lengo ni kupunguza vifo wa watoto na kusaidia kutoa
huduma bora kwa wananchi wasio na uwezo walioko katika wilaya hiyo na sehemu za jirani.
Alisema
watoto wachanga wanategemea sana misaada kutoka kwa wakubwa hivyo
msaada wa huduma bora ni jukumu la kitu mwanajamii kuweza kutoa kile
ambacho anaweza kuasaidia katika jamii.
"Tutajitahidi
kuweza kuwalinda kwa njia yoyote na moja ya malengo ya IOP ni kuweza
kulinda afya za watanzania na kuwaletea maendeleo hivyo msaada huu ni
mwanzo tu wa kuwapatia vifaa vya kazi" alisema Klaas
Klaas
alisema msaada huo ni ishara ya kuendelea kuimarika kwa ushirikiano
baina ya hospitali hiyo na asasi hiyo na kuahidi kuendelea kutoa misaada
kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa wilaya ya Kilolo.
Kwa
upande wake, Dk. Erasto Rite alisema msaada wa vifaa tiba utaisaidia
hospitali hiyo kuhudumia watoto wengi zaidi na kwa uhakika na
kuwashukuru shirika hilo lisilo la kiserikali kwa msaada huo uliowafikia
kwa wakati. Alisema hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa vifaa tiba, ukosefu wa maji, chumba cha maiti na ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa
Alisema
lengo la Hospitali hiyo ni kuongeza viwango vya matibabu kuweza kufikia
hadhi ya kitaifa kwa kuwa na vifaa bora na kuongeza huduma nyingi zaidi
ambazo hazipatikaniki katika hospitali hiyo.
Rite
alisema lengo la hospitali hiyo kupunguza vifo vya mama wajawazito na
watoto wanaozaliwa kabla ya muda (njiti) kuimarisha miundo mbinu ya
hospitali hiyo kwa kujenga idara mbalimbali na kujenga sehemu za kulaza
wagonjwa .
No comments:
Post a Comment