VIBINTI HIVI VINADAIWA KUBAKWA KWA ZAMU NA MCHUNGAJI WA KANISA LA PENTEKOSTE |
Baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Maendeleo wakizungumza kwa hisia tukio hilo la ubakaji lililofanywa na Mchungaji |
Kanisa linaloendeshwa na Mchungaji Bryson Mwaikambo |
Shule ya Msingi Maendeleo ambako wanasoma wasichana wanaodaiwa kubakwa na Mchungaji kwa zamu |
Wazazi wa watoto wanaodaiwa kubakwa na Mchungaji wakiwa katika |
Nyumba anayoishi Mchungaji Mwaikambo ikiwa imepigwa kufuri |
Kufuri!!! Ngaaa!!!! mchungaji huyooo kasepa |
Nyumba anayoishi Mchungaji Mwaikambo |
Diwani wa Kata ya Nsalala Mashauri Mbembela akitoa msimamo wake juu ya vitendo vya kinyama walivyofanyiwa mabinti hao |
Ripota Wetu
MCHUNGAJI
wa kanisa la Pentekostal aliyefahamika kwa jina la Bryson Mwaikambo(55)
anadaiwa kuwabaka na kuwaambukiza ugonjwa wa zinaa wanafunzi wawili wa
kike wanaosoma katika shule ya msingi ya Maendeleo wa kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya vijiji mkoani Mbeya.
Wanafunzi
hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri kati ya miaka 11 na 13 wanaosoma
darasa la nne na darasa la sita walifanyiwa unyama huo kuanzia mwaka
2012 ambapo alianza kujenga mazoea na watoto hao wadogo kwa kuwapa
peremende pamoja na fedha.
Imeelezwa
kuwa mchungaji huyo ambaye anaendesha ibada katika kanisa hilo dogo
lenye waumini wachache lililopo kitongoji cha kanani kijiji cha ‘Tunduma
Road’alikuwa akiwavizia watoto hao kwa muda mrefu kila walipokuwa
wanapita kuelekea shuleni.
Katika jitihada zake za kuwanasa watoto hao wa kike alimdanganya mmoja wa wazazi wa watoto aliyefahamika kwa jina la Bw.John Mussa(38)
na kumuomba binti yake awe anamsaidia kazi za nyumbani nyakati za jioni
kutokana na kuwa mke wa mchungaji kuwepo safarini.
Kwa
kuamini kuwa mchungaji huyo alikuwa ni mtumishi wa Mungu, Bw. Mussa
aliridhia mwanaye aende kuishi na Mtumishi huyo wa Mungu bila kujua
hatima ya kile ambacho kimemtokea binti yake kwa sasa.
Kwa
mujibu wa maelezo kutoka kwa wazazi na walimu wa shule ya Msingi
Maendeleo ni kwamba mabinti hao walikuwa wakifanya ngono na mchungaji
huyo kwa zamu na kwamba walianza kujua tatizo hilo baada ya kutokea
mgongano baina ya wasichana hao wawili .
‘’Tumejua
tukio hili baada ya kutokea ugomvi baina yao wa kugombania maji na
hivyo kuanza kurushiana maneno, mmoja wa watoto hao alikuja ofisini
kushitaki kuhusu ugomvi wao ndipo mmoja akasema kuwa mwenzie anatembea
na Mchungaji Mwaikambo’’alisema Mwalimu mkuu msaidizi Bi. Lucy
Kamongile.
Alifafanua
kuwa, baada ya tukio hilo walimu kwa pamoja walilazimika kuwauliza
zaidi ndipo walipoanza kujieleza kuwa wamekuwa wakilala na Mchungaji
huyo kwa muda mrefu na kwamba mwanzo alikuwa akiwapa peremende na
baadaye akaanza kuwapa fedha.
Alisema
kuwa walilazimika kuitisha kikao cha dharura baina ya wazazi wa watoto
hao na walimu ambapo walieleza tukio zima la kuingiliwa kimwili na
Mchungaji huyo tangu mwaka jana.
‘’Nililazimika
kuwaita wazazi pamoja na wanafunzi tulikaa katika ofisi ya walimu,
watoto walieleza tukio zima mbele ya wazazi wao juu ya vitendo
walivyokuwa wakifanyiwa na Mchungaji huyo.
Alisema
kuwa mara baada ya kikao hicho cha wazazi waliwapeleka watoto hao
katika kituo kidogo cha Polisi kilichopo katika mji mdogo wa Mbalizi
ambako walipewa Fomu ya Polisi Na. 3,(PF3) kwa ajili ya kuepelekwa
hospitali ili wapatiwe matibabu.
Mwalimu
Kamongile ambaye alikuwa na walimu wenzie katika ofisi ya Mwalimu mkuu
wa shule hiyo wakati akitoa taarifa hizi mbele ya Ripota Wetu kuwa
wanafunzi hao walipatiwa matibabu katika hospitali Teule ya Ifisi ambapo
kwa mujibu wa taarifa za mganga aliyewachunguza watoto hao ni kwamba
mbali na kufanyiwa ubakaji wote wawili walikuwa wameambukizwa ugonjwa wa
zinaa wa kaswende.
‘’Tukio
hili limetufedhehesha sana tulikuwa tunatafakari wapi tutaenda,tunaomba
kilio chetu kifike chama cha Waandishi wa Habari wanawake TAMWA kitoe
taarifa hizi kwa undani waone namna ambavyo jamii ya pembezoni
inavyokosa msaada na haki za kisheria,’’alisema Mwalimu Kamongile.
Mwalimu
huyo alisema kuwa wanatambua juhudi za chama cha waandishi wa habari
wanawake TAMWA ambazo wamekuwa wakizifanya hivyo wanaimani chama hicho
kikisikia suala kitalifanyia kazi kwa kina zaidi kuisaidia jamii ambayo
aina mahali pa kusemea.
Kwa
upande wa watoto hao ambao walikuwa wakizungumza kwa kupokezana juu ya
kadhia iliyowakuta walisema kuwa Mchungaji huyo alianza kufanya nao
vitendo vya ngono tangu mwaka 2012 kwa kuwadanganya kwa fedha na
peremende na baadaye wakazoea kwenda kwa Mchungaji huyo mara kwa mara.
Mwanafunzi
anayesoma darasa la nne alisema kuwa alianza kutembea na Mchungaji huyo
wakati akimpitia mwenzie aliyekuwa akiishi nyumbani kwa mchungaji
ambapo siku hiyo alimuita chumbani kwake na kumlazimisha kulala
kitandani ambapo alianza kumuingiza vidole katika sehemu zake za siri.
“Siku
ya kwanza nililia sana wakati mwenzangu yupo pembeni akishuhudia
mchungaji akinifanya na ndipo mwenzangu alisema jikaze rafiki
yangu”alisema Mtoto huyo.
Alisema
kuwa mara baada ya kumuingiza vidole alivua nguo zake na kumbaka huku
akilia wakati msichana mwenzie (alimtaja jina) akiwa amekaa pembeni ya
kitanda akimweleza kuwa aache kulia kwa kuwa baada ya kumaliza watapewa
fedha za kutumia shuleni.
Binti
huyo aliendelea kusema kuwa alipata maumivu makali wakati Mchungaji
huyo akitekeleza ubakaji wake ambapo mara baada ya kumaliza` alimpa
sh.500 na peremende na baadaye alimwita mwenzie kitandani na kufanya
naye ngono huku akishuhudia kwa macho yake.
Alisema
mara baada ya kumaliza kufanya na mwenzie Mchungaji Mwaikambo aliwaonya
wasiseme kwa wazazi wao kisha akawapa fedha na kuwaonya wasiseme jambo
hilo kwa mtu yoyote.
Akizungumza
sababu za kutosema kwa walimu au wazazi wake binti mwingine anayesoma
darasa la sita alisema kuwa Mchungaji huyo aliwatishia kuwachinja na
kuwafukia kwenye shimo iwapo atasikia wamesema tukio hilo kwa wazazi ama
walimu wao.
Alisema
kuwa Mchungaji aliwaomba wazazi wake ili aende kuishi nyumbani kwake
kumsaidia kazi kutokana na mama Mchungaji ‘’Mke wa Mchungaji’’ kuwa
safarini na kwamba katika siku hizo ndipo Mchungaji huyo alipoanza
kulala naye mahusiano taratibu.
Alisema
kwa siku za mwanzo alikuwa akimuingiza vidole katika sehemu zake za
siri na baadaye akaanza kumbaka ambapo alijisikia maumivu makali lakini
alimbembeleza kwa kumpa sh.1000 ambayo alikuwa akitumia shuleni kwa
kununua chipsi.
‘’Alikuwa
akiniingiza vidole huku chini(akionyesha sehemu za siri) akanibaka,
sikuweza kumwambia baba niliogopa atanichinja..mwenzangu alipokuwa
anakuja kunipitia kwenda shuleni naye alianza kumuingiza vidole
akambaka!!, alilia sana, nikamwambia asilie atatupa hela,’’alisema.
Alisema kuwa wamebakwa na Mchungaji huyo zaidi ya mara nne na kila alipokuwa akiwabaka alikuwa anawapa hela za kutumia shuleni.
Kwa
upande wazazi wa watoto hao Bw.Suveli Harrison na Bw. John Mussa
walikiri kuitwa shuleni na kupata taarifa za kubakwa kwa watoto wao
walipoitwa shuleni ambapo watoto walijieleza walichokuwa wakifanyiwa na
Mchungaji Mwaikambo mbele ya walimu.
‘’Jambo
hili lilitushitua sana, machozi yalitulenga, hatukutegemea kusikia
Mchungaji anaweza kuwabaka watoto ambao ni sawa na wajukuu zake,
tulienda polisi walitupa karatasi tukaenda Hospitali ya Ifisi, watoto
walikutwa na maambukizi ya ugonjwa wa zinaa,’’alisema Bw. John Mussa.
Alisema
kuwa yeye aliridhia mwanaye kuishi na Mchungaji huyo baada ya kuombwa
kutokana na mchungaji huyo kuishi na mtoto mdogo wakati mkewe akiwa
safarini.
Bw.
Mussa alisema kuwa hakujua kuwa kama kuna siku mwanaye atadhurika kwa
kufanyiwa kitendo cha unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kama
walivyofanyiwa watoto hao na kwamba hata hivyo hadi sasa hakuna jitihada
zozote za jeshi la polisi zilizofanikisha kumnasa Mchungaji huyo.
Alisema
kuwa kwa sasa watoto hao wamekuwa wakitishiwa na Mchungaji kutokana na
kufahamika kuwa yeye aliwabaka na kwamba anaomba msaada wa kisheria
kusimamia haki ili sheria iifuatwe dhidi ya mtuhumiwa wa ubakaji.
Naye
mzazi mwingine Bw.Suvile Harrison alisema kuwa hakujua chochote juu ya
vitendo alivyofanyiwa mwanaye na Mchungaji huyo na kwamba alifahamu
tukio hilo baada ya kuitwa shuleni ambako walimu waliwaita watoto wao na
kueleza tukio zima walilokuwa wakifanyiwa na Mchungaji.
Alisema
kuwa hakubaini mabadiliko yoyote kwa mwanaye juu ya vitendo
alivyofanyiwa na wala hajawahi kuhisi lolote hadi hapo alipoitwa shuleni
na walimu.
Baada
ya taarifa hizo waandishi wa habari wa gazeti hili walifunga safari
hadi katika nyumba ambayo inasadikiwa kuwa ndipo anapoishi Mchungaji
huyo na kukuta mlango ukiwa umefungwa lakini alijitokeza jamaa ambaye
alijitambulisha kuwa ni mmiliki wa nyumba hiyo Bw. Zacharia Gambi.
Bw.Gambi
alisema kuwa anamfahamu mpangaji wake kwa jina moja la Mchungaji
Mwaikambo na kwamba mbali ya kuwa ni Mchungaji wa Kanisa la Kipentekoste
ni Balozi wa nyumba kumi wa mtaa wa Kanani.
Bw.Gambi
alisema kuwa Mchungaji huyo hajaonekana muda mrefu na kwamba mkewe
amekuwa na desturi ya kuondoka alfajiri kuelekea shambani na kurudi
usiku.
Kadhalika
imeelezwa na baadhi ya watu ambao hawakupenda kutajwa majina yao
gazetini kuwa kitendo cha Mchungaji huyo kuwabaka mabinti wadogo
kimetokana na imani za nguvu za giza kwamba kwa kufanya hivyo
kitamuongezea waumini katika kanisa lake dogo lililopo katika mtaa wa
Kanani.
Mama
mzazi wa mmoja wa watoto waliobakwa aliyejitambulisha kwa jina la Jane
John(35) alisema kuwa awali yeye alikuwa ni mmoja wa waumini katika
kanisa hilo lakini baadaye walihamia kanisa jingine baada ya kuona
mienendo ya mchungaji huyo kutofanana na kazi ya huduma za kiroho.
Alisema
waumini wengi wamehama katika kanisa hilo wakiwemo watoto wake wakubwa
wa kike ambao walieleza waziwazi tabia ya ukware ya Mchungaji huyo ya
kuwafuatilia mabinti wadogo kwa ajili ya kufanya nao vitendo vya ngono.
Diwani
wa Kata ya Nsalala iliyopo Mbeya vijijini Bw.Mashauri Mbembela
alipozungumza na waandishi wa gazeti hili alisema kuwa anashangazwa
tukio hilo kutoshughulikiwa kwa kipindi chote huku taarifa zikiwa
zimefikishwa kituo cha polisi.
Alisema
kuwa tukio hilo ni la unyanyasaji ambalo lilipaswa kushughulikiwa kwa
nguvu zote na kwamba kuna haja ya kuweka sheria ngumu itakayokomesha
vitendo vya ubakaji kwa watoto wa kike.
Bw.Mbembela
alisema kuwa ili kukomesha tabia za ubakaji, itungwe sheria ya kuwahasi
wabakaji badala ya kuwafunga jela miaka 30 ambako wanaenda kula
chakula kinachotokana na kodi za wananchi.
‘’Wabakaji
wanafungwa jela, wakimaliza vifungo vyao hurejea uraiani ambako
wanaweza kuendeleza vitendo hivyo, njia pekee ya kukomesha ubakaji ni
kuwahasi, wakirudi uraiani wataendeleza kujenga Taifa,’’alisema Bw.
Mbembela.
Ripota
wetu alifanya jitihada za kutafuta namba za simu za mchungaji huyo
ambaye mara baada ya kupokea na kuulizwa juu ya tuhuma hizo alikanusha
na kusema kuwa huu ni uzushi na uongo uliolenga kumpaka matope ili
kuchafua huduma zake anazotoa kwa waumini .
Alidai
kuwa kanisa lake la Pentecostal Holiness lenye jumla waumini nane
linatoa huduma za uhakika kijijini hapo hivyo baadhi ya wafuasi wa
shetani wanalipiga vita ili lisiendelee kukua ili kuwafikia wanakondoo
wengi.
“Wananipakazia
tu unaweza kuingiwa na ibilisi na hivi ulivyonipigia nafikiria kuchukua
maamuzi magumu na mwili wangu hamtauona kamwe bora uliwe na ndege na
wanyama wa porini niende jehanamu kuliko kuchafuliwa huku”alisema
Mchungaji huyo.
Kwa hisani ya Mkwinda Blog
No comments:
Post a Comment