Ili
kumuwezesha Rais Jakaya Kikwete na wageni wengine akiwemo Makamu wa
Rais DK Mohamed Bilal na Rais wa Zanzibar DK Mohamed Shein kuweza
kuingia Bungeni leo, bunge limetengua kanuni ya 153 ikiwa ni moja ya
Kanuni za Bunge toleo la 2003 ili viongozi hao wahudhurie Mkutano wa 13
kikao cha nane.
Mnadhimu Mkuu wa Serikali Waziri WILLIAM LUKUVI amesema kwa
kutenguliwa kanuni hiyo na ile ya 31, wageni wataruhusiwa kukaa sehemu
ya spika ambapo Rais JK atalihutubia bunge la kumi kwa mara ya pili.
Namkariri Spika Anne Makinda akisema ‘itakumbukwa hii ni mara ya pili
kwa Rais kutuhutubia sisi na tuna utaratibu wa Mihimili kwa hiyo hoja
hii naomba tutengue kifungu cha wageni wasiokua wabunge wasiingie humu
ndani sasa, hawa tuwakaribishe’
Baada ya hiyo sentensi, Spika aliuliza maswali ya wanaounga mkono na
wasiounga mkono ambapo japo kuna waliosema sioo, waliotoa jibu la ndio
ndio walishinda kutokana na wingi wao.
NA : MWIGULU NCHEMBA BLOG
No comments:
Post a Comment