skip to main |
skip to sidebar
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, JOHN CASMIR MINJA AMVISHA CHEO CHA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA MAGEREZA AFISA MWINGINE ALIYEKUWA ANAHUDUMU ULINZI WA AMANI KATIKA JIMBO LA DARFUL – SUDANI LEO JIJINI DAR
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akimvisha Cheo
cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge
ambaye anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful – Sudan.
Hafla ya uvalishaji cheo imefanyika leo Novemba 18, 2013 katika Ukumbi
wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( kulia) akimpongeza
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge mara
baada ya kumvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza leo
katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini
Dar es Salaam. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus
Clement Marenge ni miongoni mwa Maafisa wa Jeshi la Magereza ambao
wanahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful – Sudan.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimpongeza Dkt. Deus
Clement Marenge(wa tatu kulia) kwa kutosi vinywaji kama inavyoonekna
katika picha mara baada ya hafla fupi ya uvishaji cheo kwa Afisa
Mwandamizi wa Jeshi la Magereza ambaye amevishwa cheo cha Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini,
John Casmir Minja(hayupo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa nasaha fupi mara
baada ya zoezi la uvalishaji cheo kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Dkt. Deus Clement Marenge( hayupo pichani) ambaye kwa sasa
anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful – Sudan.
Kamishna
wa Magereza wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(aliyesimama)
akimpongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Deus Clement
Marenge mara baada ya zoezi la uvalishaji cheo lililofanyika leo
Novemba 18, 2013 katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la
Magereza, Jijini Dar es Salaam( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza
No comments:
Post a Comment