Actress Elizabeth Michael(Lulu) ametoa msaada wa pesa katika hospitali
ya Ocean Road jijini Dar es salaam ili ziwasaidie wagonjwa wa kansa.
Haijajulikana star huyo wa filamu ametoa kiasi gani na aliambatana na
mama yake mzazi katika hospitali hiyo. Kupitia Instagram Lulu ameandika
"naamini mimi sio mwema sana mpaka Mungu akaniwezesha kuona mwezi huu
nikiwa mzima na mwenye afya. Kwa kutambua hilo nimeanza mwezi huu kwa
kupita katika hospitali ya Ocean Road na kutoa mchango ili kuwasaidia
wagonjwa wa cancer na tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa
chochote tulichonacho"
Mungu awe upande wako na akuzidishie zaidi Lulu
Lulu akiwa na mama yake mzazi akitoa msaada wa pesa katika hopspitali ya Ocean Road...
No comments:
Post a Comment