SEKUNDE
chache kabla ya mwamuzi Mohamed Theofile wa Morogoro hajamaliza pambano
la Ligi Kuu ya Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, mashabiki
wanaodhaniwa kuwa ni wa Simba, wamevunja viti zaidi ya 100 na kuvirusha
uwanjani imefahamika.
Mwandishi
wa mtandao huu alishuhudia mashabiki hao wakivunja na kuvirusha
uwanjani viti hivyo baada ya mwamuzi huyo kuwapa Kagera penalti
iliyofungwa na Salum Kanoni.
Mashabiki
hao ambao licha ya kuwa walikaa katika majukwaa tofauti, waliweza
kufanya kitendo hicho kwa kile kilichoelezwa baadaye kwamba ni kupingana
na maamuzi ya mwamuzi huyo.
Viti vilivyovunjwa vingi vina rangi ya chungwa na bluu ambavyo kwa haraka haraka idadi yake inaweza kuwa zaidi ya 100.
Kutokana
na hali hiyo, askari wa Jeshi la Polisi walilazimika kulipua mabomu
matatu ya machozi ili kuwatuliza mashabiki hao walioonekana kuwa na
hasira.
Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura ameuambia
mtandao huu kwamba, kwa kitendo hicho kamati ya mashindano na ile ya
nidhamu zinaweza kukaa na kutathimini uhalibifu uliofanywa na mashabiki
hao kisha timu husika kuwajibika kulipa.
“Kila
mtu ameona kilichotokea na vurugu za kuvunja viti zilianza tangu wakati
wa mapumziko hivyo uchunguzi utafanyika na klabu iliyohusika italipa
faini kama utaratibu ulivyo,” alisema Wambura kwa kifupi.
|
Kipa
wa akiba wa Simba, Abel Dhaila, akimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya
mwamuzi wa kati kutoa penati katika dakika za majeruhi.
Kipa wa akiba wa Simba, Abel Dhaila, na Kocha Mkuu, Abdallah Kibaden,
wakimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya mwamuzi wa kati kutoa penati
katika dakika za majeruhi.
Wachezaji wa akiba wa Simba wakisikitika baada ya kuamuliwa kupigwa penati hiyo.
Askari wakiendelea kumdhibiti shabiki aliyekamatwa baada ya mashabiki hao kuvunja viti na kuanza kuruka uwanjani.
Askari wakiendelea kudhibiti vurugu..
Sehemu ya viti vilivyoharibiwa....
No comments:
Post a Comment