Leo tarehe 03/11/2013 Mhe Freeman Mbowe alifika katika Wilaya ya
Bunda kuhani msiba wa Mzee Zamberi Ngobai aliyekuwa Diwani wa Kata ya
Nyasura iliyoko Bunda Mjini kwa tiketi ya CHADEMA.
Diwani huyo alifariki dunia tarehe 28/10/2013 akiwa katika hospitali
teule ya Bugando ambako alilazwa kwa matatizo ya ugonjwa wa Kiharusi.
Mhe Freeman Mbowe aliongozana na msafara mkubwa wakiwemo, Mhe.
Lwakatare, Esta Matiko (Mb), Meshack Opulukwa (Mb), Recho Mashishanga
(Mb), John Mrema na viongozi wa Mkoa na wa Kanda. Familia ya marehemu
imeshukuru kwa jinsi ambavyo chama kilionesha ushirikiano mkubwa tangu
ugonjwa hata mauti.

No comments:
Post a Comment