Wiki
chache baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha kutimuliwa
kwa madai ya kukihujumu chama hiho, leo jioni Mbunge waMaswa Magharibi, John Shibuda ametimuliwa katika kikao cha Kanda ya Ziwa Mashariki kwa madai ya usaliti.Kikao
hicho ambacho kinaendelea kufanyika mkoani Shinyanga katika Hotel ya
Karena, kinajumuisha wajumbe wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara
inayounda Kanda ya ziwa Mashariki.Hali ilianza kumbadilika baada ya
viongozi wa kitaifa wakiongozwa na mwenyekiti wa Taifa wa Chadema
Freeman Mbowe, kufika ukumbini hapo ambapo majira ya saa 1:00 jioni,
jumbe mmoja alisimama na kutoaa hoja kuwa kikao hicho hakiwezi kuendelea
kujadili masuala ya msingi ya chama ilihali kikiwa na watu ambao
wanatoa taarifa CCM.Mjumbe huyo, alibainisha wazi kuwa mtu anayemkusudia
katika kikoa hicho ni Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chadema
John Shibuda, ambaye alisema amekuwa akisimama katika mikutano ya CCM na
kuhutubia huku akijiita mwana Chadema.Alieleza hivi karibuni, Mbunge
huyo alikuwa katika kikao cha CCM ambapo alisimama kihutubia mbele ya
Nape na kudai kua vyama vya wapinzani havina kitu na kwamba CCM ndicho
chama Tawala.
“Hatuwezi
kuendelea na kikao hiki tukiwa tunajadili masuala ya kwetu wakati
tunaye mtu anayetupinga hadharani kwa mwenendo wake na matendo yake
bora, Shibuda huyu katika mkutano wa CCM Meatu mbele ya Nape na Kinana,
alisimama jukwaani na kuisifia CCM kuwa ndicho chama makini na wapinzani
ni watoaji matusi tu, hivyo napendekeza atupishe kwa amani,”
alikaririwa mjumbe huyo akimtaka Mbowe kumwondoa Shibuda katika mkutano
huo.
Kutoka na
hoja hiyo wajumbe ndani ya mkutano huo waliunga mkono na wote kutaka
atolewe hali iliyomfanya Mwenyekiti Mbowe kuwasihi wajumbe kumpa nafasi
ya kujieleza kwa vile ni kiongozi na kubanisha kwamba hakuja hakuja
kufukuza mtu katika kikao hicho.
Baada ya
hooja hiyo ya Mbowe wajumbe walitulia na ndipo Mwenyekiti alipompa
nafasi ya kujieleza na kudai kuwa CCM ni chama tawala na kutoa misemo na
mifano kadhaa hali ambayo ilizua kelele za wajumbe wakimtaka kutoka nje
na misemo yake.
Aidha
katika utetezi wake Shibuda alisema kwamba mtu mzima unapokuwa na shida
yoyote unakwenda kwa Baba yako, CCM ni chama Tawala hivyo yeye anakiona
kama Baba yake hasa napokuwa na matatizo Jimboni kwake.
Kauli hii ilionekana
kuwaudhi zaidi wajumbe wa kikao hicho na kuanza kumshambulia kwa maneno
hali ambayo ilimfanya Mbowe kuingilia kati na kuwataka wajumbe kupiga
kura iwapo wanakubaliana na ama abaki katika kiako ama atoke na wajumbe
wengi kuwa upande wa atimuliwe huku akiambulia kura 2 za kumtaka abaki
katika kikao. Hivyo majira ya saa 1:23 jioni Mbowe alimwomba atoke nje
ya kikao hicho na kuheshimu kura za wajumbe hao na hoja hiyo kuishia
hapo na kikao kuelendea.CHANZO AUDIFACE JACKSON
No comments:
Post a Comment